Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwafuta machozi wazazi waliokuwa wanashindwa kugharamia elimu ya kidato cha tano na sita nchini.
Kauli hiyo ya shukrani ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthonty Mavunde alipokuwa akitoa salamu kwa wananchi katika hafla ya kukabidhi vifaa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa shule ya sekondari Chinangali tukio lililofanyika shuleni hapo.
Mavunde alisema “sisi Halmashauri ya Jiji la Dodoma tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais. Rais amewafuta machozi wazazi wengi waliokuwa wanashindwa kugharamia kidato cha tano na sita. Hivyo, elimu bila ada itakuwa hadi kidto cha sita. Kazi ya mzazi itakuwa ni kulea mtoto na akinza shule serikali serikali inaendelea” alisema Mavunde.
Mavunde ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo aliwataka vijana kujiandaa na program yake ya kusaka vipaji “Mavunde talent seach” ambapo vijana wanaofanya vizuri wanapata fursa ya kusomeshwa. “Mwaka uliopita Watoto zaidi ya 20 nimewapeleka shule ya Ellen White kidato cha kwanza hadi cha nne” alisema Mavunde.