Asilimia 99 ya ubaguzi wa mtoto shuleni umetokomezwa na serikali ambapo wadau wanakumbushwa juu ya kutatua changamoto zinazowakabili Watoto kwa zingati uwepo wa Sera muhimu za kuwapatia Watoto huduma Bora Kama elimu afya na Mambo mengine yanayofaa katika jamii.
Hayo yameelezwa na meya wa manispaya ya Bukoba mh. Gibson Godson katika maadhibimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyoka katika viwanja vya mashujaaa mayunga mjini Bukoba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Tuimalishe ulinzi wa mtoto tokomeza ukatili dhidi yake,jiandae kuhesabiwa ambapo amewakumbusha wazazi na wadau pamoja na serikali kuhusu wajibu wao wa kuendelea, kusimamia Sera na kanuni za kuwalinda Watoto bila kuwabagua na inatoa hamasa kwa jamii kwa watanzania wote kuendelea kujiandaa kuesabiwa.
Pia amewataka Watoto kuendelea kuibua vitendo vya kiukatili vinavyowakumba kwani vipo vyombo vya kutetea haki zao Kama madawati ya Watoto, mahakama na mamlaka nyingine, kupitia lisala iliyosomwa na Watoto amesema kuwa manispaa ya bukoba itaendelea kusimamia na kutatua changamoto zinazowakabili na manispaa itahakikisha kupitia serikali ya awamu ya sita wanapatiwa madawati shuleni, viti sambamba na meza .
Aidha ametoa maagizo kupitia afisa elimu wa manispaa ya Bukoba kuhakikisha Walimu huko shuleni endapo mtoto akikosea asichapwe chini ya viboke 4 kwani vikizidi Ni unyanyasaji na kuagiza pia kuhakikisha shule zote zinakuwa na madarasa ya awali.
“Kwa Sasa ipo Sera ya kupanda miti ya matunda shuleni Sasa Basi kupitia siku hii ya leo nakuagiza afisa elimu kuhakikisha shule zote manispaa ya Bukoba wanapanda Miche ya parachachi kuanzia Miche 50 na kuendelea”alisema Meya.
Pia ameagiza kuhakikisha Watoto wote shuleni wanapata uji kupitia mkurugenzi ametoa siku 14 kwa viongozi hao kuja na mkakati wa kujua ni jinsi gani Watoto wote watapata uji shuleni na kuwashirikisha wazazi katika vikao jinsi ya kuchangia zoezi Hilo kwa watoto waweze kupata uji shuleni.
Nao wanafunzi wakasilisha Shukrani zao kwa serikali kupitia lisala iloyosomwa na Noeli Chalanja mwanafunzi wa shule ya sekondari Bukoba ambapo amesema bado Watoto wanazo changamoto nyingi zinazowakabili licha ya serikali kuendelea kuzitatua bado uboreshaji wa huduma za Watoto kwa kujengewa miundombinu ya shule na majengo maalumu ya kujisiti iri kwa Watoto wa kike pindi wawapoo kwenye hedhi na mabweni kwa ajili ya kupunguza vtendo vya kubakwa pindi wawapoo njiani kuelekea shuleni.
Licha ya uwepo wa changamoto hizi pia wameomba kuwepo kwa bunge la Watoto ili kuwezesha kushirikishwa katika utoaji wa maamuzu, wameongeza kuwa ipo haja ya somo la kingereza kufundishwa kuanzia darasa la awali kuliko kuanzia darasa la tatu Jambo ambalo linapelekea kuferi kwenye mtihani wa taifa wa darasa la nne, lakini pia wanafunzi wengi kurundikana katika Madarasa na kupelekea kuwepo kwa ufaulu hafifu, Watoto kutelekezwa na mwisho wa siku kuwa Watoto wa mtaani na kumalizia kwa kuiomba serikali kuwasaidia watoto wanaomaliza darasa la Saba na kushindwa kuendelea na shule kuomba kupelekwa katika vyuo vya ufundi ili kupunguza makundi ya kiarifu mtaani.
Nae afisa maendeleo ya jamii ndg .Wanchoke Chinchibera amesema wakati anawisilsha taarifa ya utekeleza wa Sera ya mtoto kuwa Upo ukatiri wa kijamii ambapo wazazi uwafungia Watoto ndani na kuwaoza Watoto kike wakiwa katika umri mdogo katika kutekeleza na kuzitambua haki za Watoto imetolewa elimu kwa wanafunzi 2485 juu ya elimu ya uzazi na hedhi salama kwa baadhii ya shule ikiwemo shule ya sekondari rugambwa wanafunzi 672, kagemu sekondari wanafunzi 490, mgeza wanafunzi 709, Katika kulinda haki za Watoto kitengo Cha idara ya jamii kimejitaidi kumaliza kesi hizo .
Hata hivyo amesema zipo Changamoto kwa baadhii ya wazazi kutotimiza majukumu yao ya kulinda Watoto na kupelekea Watoto kuwa wengi mtaani lakini pia lengo la manispaa ya bukoba Ni kuhakikisha kabisa vitendo vya kiukatili kutokuwepo kwa watoto kabisa.