Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KAMATI ya Usalama wilaya ya Kibaha ,imetoa onyo na kupiga marufuku baadhi ya wafugaji wanaodaiwa kutumia vibaya silaha na kutishia wasio na hatia ,kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa amani na kinyume Cha matumizi.
Aidha imerejea onyo Hilo, kwa matumizi mabaya ya silaha za jadi Kama mishale na upinde na endapo kutatokea tukio la aina hiyo kamati hiyo haitosita kukomesha matumizi ya silaha hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama wilaya,Sara Msafiri alitoa maagizo hayo baada ya kufika Kijiji Cha Kitomondo ,Kata ya Ruvu Mkoani Pwani na kupata taarifa juu ya baadhi ya wafugaji wavamizi wanaotishia wakulima na wafugaji wengine kwa silaha mbalimbali huku wakiingiza mifugo kiholela kutoka ng’ambo.
Alisema ,kibali Cha kumiliki silaha hakiruhusu Raia kutishia Raia mwingine silaha ,hivyo waaanza kutafakari umiliki wa silaha kwa watu wa aina hiyo .
“Migogoro yenu malizeni kwa kukaa chini na kuheshimiana,bila ya kutumia bunduki,mishale Wala upinde.”
Sara alisema ,anayachukua majina ya waliohusika na tukio Hilo ili vyombo vya sheria vikaendelee na uchunguzi na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho ndani ya jamii.
“Acheni kuweka sheria mfukoni,achane kudharau vyombo vya sheria, kisa rushwa ,”sitovumilia mambo haya katika wilaya hii,”;Natoa Rai na kwa Serikali za vijiji, maofisa mifugo kufuata na kusimamia Utaratibu wa wafugaji kuingia katika vijiji .”alisisitiza.
“Kuna wasiwasi hapa ,Kuna mianya ya rushwa ndio inayotafuna Kijiji haiwezekani wafugaji wanaingia watakavyo na kuweka sheria mifukoni wakati wananchi mpo na Serikali ya Kijiji na kata mpo”
Pamoja na hayo,Sara alikemea mifugo holela na kuagiza Serikali ya kijiji cha Kitomondo kukutana na wafugaji wiki ijayo ili kubaini wafugaji wavamizi na idadi ya wafugaji wanaotambuliwa kuomba kibali Halali kwa mkutano wa Kijiji .
Vilevile mkuu huyo wa wilaya ,aliielekeza kamati ya usuluhishi ya kijiji na ofisa mifugo kupitia maboma yote ili kubaini wananchi wanaokodisha wafugaji ardhi .
Aliwataka wananchi kuheshimu juhudi za Serikali wakati ikileta Suluhu na kusimamia changamoto za wakulima na wafugaji wao wanakwenda kuwakumbatia wafugaji na kuwakodisha ardhi Hali inayosababisha migogoro isiyoisha.
Wakulima wa Kitomondo ,Kidawa Omary ,Hamza Botea Walisema ,kumezuka wimbi la mifugo na wafugaji wavamizi Hali inayosababisha kuliwa mazao Yao na kupata hasara .
Kidawa alisema , mfugaji Dotto Mabula ana maboma mengi ya Mifugo na ndio tishio la wafugaji.
Mfugaji Michael Mjika alisema ,Chama Cha wafugaji huwa kina kutana na kujadili changamoto zao ,ambapo amekiri kuwepo kwa wafugaji wavamizi na ambao wanakiuka taratibu na sheria mbalimbali.
Michael Lobe ambae amepigwa na baadhi ya watu waliotumwa na mfugaji ambae amedaiwa kuwa mbabe Dotto Mabula alisema, Juni 9 alivamiwa na kupigwa na kutishiwa bunduki wakati alipokwenda kumtembelea mkulima mmoja ambae amemkodisha ardhi kuweka mifugo.
Ofisa mifugo kata ya Ruvu ,Fransis Ekoni alipokea maagizo hayo na kusema wafugaji wanaotambulika katika kijiji cha Kitomondo ni wanne tu.
Ombeni Msangi kaimu mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kibaha,alieleza kuwa, kuingiza mifugo eneo jingine, Kijiji kingine kwa wakulima ni kosa.