Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbas wakipata picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuwasili hii leo Juni 16,2022 katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpokea Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuwasili hii leo Juni 16,2022 katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akipata picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuwasili hii leo Juni 16,2022 katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akimpokea Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuwasili hii leo Juni 16,2022 katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbas amempokea Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin ambapo amewasili kwaajili ya kufanya ziara ya kiiman na mapumziko mafupi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 16,2022 mara baada ya kumpokea kiongozi huyo, Waziri Mchengerwa amesema amewasilisha kwa kiongozi huyo salaam za Rais Samia ikiwemo utayari wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mhadhara mkubwa wa mwaka wa kiongozi huyo utakaoleta maelfu ya watu hapa nchini.
“Hii ni sehemu ya muendelezo wa Royal Tour (post royal tour) ambapo Mhe Rais wetu amefanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi yetu na sasa wawekezaji na watalii wakiwemo viongozi wa kimataifa wa kiimani na wa kijamii nao wanazidi kuja Tanzania. Kwa eneo letu sisi la utamaduni tumemhakikishia Sheikh kuwa Tanzania ni salama na aendelee kutuombea amani lakini pia alete wafuasi wake wengi zaidi kuja kutembelea na kuwekeza Tanzania,” .Amesema Waziri Mchengerwa.
Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa dhehebu hilo nchini Bw. Zainuldeen Adamjee amesema Saydna Mufaddal, atakuwa nchini kwa takribani wiki mbili ambapo pamoja na shughuli za kiimani amekuja kuunga mkono azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza na kuifungua nchi hasa kupitia filamu ya Royal Tour.
Amesema kiongozi huyo amekuja kuunga mkono malengo ya Royal Tour na yeye mwenyewe na wafuasi wake watakuwa na mapumziko hapa nchini na msafara wake wote baadae watatembelea katika maeneo mbalimbali na pia iwapo taratibu zikikamilika na akaridhia anaweza kufanya mhadhara wake mkubwa wa kidini Julai hapa nchini ambapo wafuasi wake kati ya 30,000 hadi 40,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani humfuata.
“Hata Hivyo kitokea tutawaonesha watu hao na mabohora wengine duniani filamu ya Royal Tour,” Amesema Bw. Adamjee.