Waziri wa Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima,aakisisitiza jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Zainab Chaula,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Stanslaus Nyongo ,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya watoto wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima (hayupo pichani),wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
Mdhibiti Ubora Haki Elimu Dk.Ellen Otaru,akitoa taarifa wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na nje ya Shule yaliyofanyika leo Juni 16,2022 jijini Dodoma.
……………………………………….
Na Alex Sonna-Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima,amesema kuwa wameanzisha Mpango kazi wa Taifa wa kupambana na vitendo vya ukatili dhidi watoto vinavyofanyika mtandaoni kwa kuandaa machapisho au majarida ya kufundishia Watoto, Wazazi na Walimu kuhusu ukatili wa Watoto mtandaoni.
Hayo ameyasema leo Juni 16,2022 jijini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kilichoambatana na uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Mwongozo wa Taifa wa Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto Ndani na Nje ya Shule.
Dkt.Gwajima amesema kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi, Tanzania katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa katika jeshi la Polisi ni 11,499 ikilinganishwa na matukio 15,870 katika kipindi kama hicho mwaka 2020 ambapo upungufu ni matukio 4,371 sawa na asilimia 27.5.
Ametaja Mikoa iliyoongoza kwa vitendo vya ukatili wa watoto kuwa ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Mkoa wa Kipolisi Ilala (489) huku makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa yakiwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114).
“Utafiti wa serikali na UNICEF unaonesha asilimia 60 ya matukio yanatokea nyumbani na asilimia 40 yanatokea mashuleni,tukumbuke, kuna uwezekano mkubwa kwamba matukio ya ukatili yanaweza kuwa mengi kuliko haya ukizingatia kwamba haya ni yale tu yaliyotolewa taarifa kwenye vituo vya polisi,”alisisitiza
Hata hivyo amesema pamoja na jitihada mbalimbali za kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto, ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ukatili kuchukuliwa hatua kali za kisheria, bado ongezeko la taarifa za vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali vinaongezeka ikiwemo Ubakaji, Ulawiti, Utumikishwaji wa watoto katika ajira hatarishi, Ukeketaji, Ndoa na mimba za utotoni na vitendo vingine vya ukatili.
Amesema katika kuongeza nguvu na kasi ya kupambana kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto na jamii kwa ujumla, wizara kwa kushirikiana na wadau wake zikiwemo wizara mbalimbali za kisekta wanaratibu kampeni shirikishi ya jamii inayoenda kwa jina la SMAUJATA (Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, 2022)dhana ya Kampeni hiyo ikiwa ni kuandikisha wanachama wengi zaidi kutoka ngazi zote na mitandao yote ya jamii wanaokerwa na uwepo wa ukatili, wenye moyo wa kujitoa bila ujira wowote kwenye kuelimisha jamii ili ifahamu juu ya uwepo wa ukatili na athari za ukatili na hatua gani wachukue kabla ya ukatili kufanyika .
“Kampeni hii na dhana yake imepokelewa na jamii kwa mwitikio mkubwa na mtazamo chanya kiasi kwamba hadi leo wameshajiunga karibu watu 5000 tena wengi wanaotaka kujiunga hawana simu janja ili kuifikia fomu ya usajili,utaratibu mzuri zaidi unaandaliwa kuwezesha watu wengi kujiunga;
Mwitikio huu maana yake ni kuwa, jamii iko tayari kwa mabadiliko na iko tayari kuwezesha mabadiliko hayo yatokee. Aidha, mwitikio huu ni faida kwetu kwenye kuziba changamoto ya rasilimali fedha na watenda kazi na kinachotakiwa kwetu sisi ni kujitoa kwenye kufanya uongozi ili hawa wasaidizi huru watimize kiu yao ya kupambana na ukatili kwenye jamii,”amesema.
Dkt.Gwajima ametaja hatua zilizochukuliwa na Wizara hiyo kukabiliana na aina mpya ya Ukatili Dhidi ya Watoto Mitandaoni unaosababishwa na kukua kwa Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na kueleza kuwa zipo jitihada kadhaa ikiwemo,Kuunda kikosi kazi cha /?Taifa cha Ulinzi na Usalama wa Mtoto mtandoni kikiwa na lengo la Kuhakikisha watoto wako salama wakiwa mtandaoni.
Pia ameeleza Chimbuko la Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo amesema imetokana na azimio la Umoja wa nchi za Afrika (OAU) la mwaka 1991 lililokuwa na lengo la kuwaenzi Watoto kutoka shule mbalimbali za nchini Afrika Kusini hususani Kitongoji cha Soweto waliouawa kinyama na Polisi wa Serikali ya Makaburu tarehe 16 Juni,1976.
Ameeleza kuwa Watoto hao wanaokadiriwa kufikia 2000 waliuawa wakati wanaandamana kupinga elimu ya kibaguzi dhidi ya watoto wenye asili ya kizungu wakiwa wanashinikiza elimu itolewe kwa usawa na kuzingatia lugha yao ya asili ili washiriki vema katika kupata elimu bora na kwamba toka kipindi hicho, maadhimisho haya yamekuwa yakitumika na Serikali na wadau katika nchi za Afrika kuelimisha na kuwakumbusha Wazazi, Walezi na jamii wajibu wao katika kuwapatia watoto haki zao za msingi zikiwa pamoja na Lishe bora, Malazi, Ulinzi, Elimu na Huduma za afya.
Aidha amesema kuwa katika kuimarisha utekelezaji wa haki, ulinzi na ustawi wa mtoto nchini, Serikali imeendelea kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na iliandaa Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 ambayo imeainisha Haki tano (5) za Msingi za Mtoto ambazo ni Haki ya Kuishi, Kulindwa, Kuendelezwa, Kushiriki na haki ya Kutobaguliwa na kwamba Wizara imeratibu utungwaji wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na sasa inafanyiwa mapitio katika baadhi ya vipengele pamoja na kanuni zake ili ziweze kukidhi mahitaji ya sasa katika utoaji wa haki kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa mtoto nchini.
“Serikali imefanya marekebisho kwenye baadhi ya vifungu vya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 kwa kuongeza kipengele kinachotoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 30 kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi au kuhusika katika kukatisha masomo yake kwa kumuozesha / kumuoa,
“Serikali na Wadau tunatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Watoto (2017/18-2021/22) ambao umewezesha kuanzishwa kwa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto 18,186 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara,tumeweza kuanzisha Dawati la Jinsia na Watoto katika vituo vyote 427 vya polisi kwa lengo la kupokea taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto na watuhumiwa kuchukuliwa hatua za kisheria,”amesema Dkt.Gwajima.
Vilevile amesema Serikali imeweza kuongeza idadi ya Mahakama za kusikiliza mashauri ya watoto kutoka mahakama 3 kwa mwaka 2015/2016 hadi kufikia Mahakama 141 Januari 2022 na kwamba wameweza kuratibu na kusimamia uanzishaji wa Vituo vya Mkono kwa Mkono (One stop Centres) na kuratibu utoaji wa huduma kwa manusura wa ukatili katika Vituo hivyo hapa nchini.
“Hadi kufikia Februari 2022, jumla ya Vituo vya Mkono kwa Mkono 20 vimeanzishwa katika Hospitali za Serikali ambazo ni Amana, Mwananyamala, Tumbi, Iringa, Sekou Toure, Mbeya FFU, Simiyu, Shinyanga, Kahama, Hai, Kitete, Mount Meru, Nindo, Kasulu TC, Kasulu DC, Kibondo DC, Kituo cha Afya Chanika (Ilala CC), Kituo cha Afya Sabasaba (Morogoro MC), Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan (Morogoro MC) na Mvomero DC na tumeendelea kutoa huduma za msingi na hifadhi ya dharura kwa manusura wa ukatili katika Nyumba Salama tisa (9) zilizoanzishwa katika Mikoa ya Arusha (2), Iringa (1), Kigoma (1), Mara (2), Manyara (1), Morogoro (1) na Mwanza (1),”amefafanua
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Zainab Chaula ametoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katika Mikoa na Halmashauri zote kuimarisha utoaji wa elimu ya malezi na makuzi ya watoto kwa wazazi na walezi ili waelewe wajibu wao wa kulea watoto kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa wa kijinsia.
“Waelekezini waazazi na walezi kuwasimamia watoto wao kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kielektroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika mitandao,usalama wa watoto ni muhimu wakati wote na hivyo, watoto wakiwa nyumbani katika kipindi hiki wajiepushe kwenda kwenye maeneo yatakayohatarisha usalama wao,”amesema
Amesema msingi mkuu wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni utoaji wa Haki za Mtoto kama ilivyoelekezwa na Umoja wa Afrika katika Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa mwaka 1991 na kwamba umoja huo umetohoa maazimio hayo kutoka katika Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989.
Siku ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka June 16,2022 na Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu inaelekeza “Tuimarishe ulinzi wa Mtoto; Tokomeza Ukatili Dhidi Yake: Jiandae kuhesabiwa” ikiwa inasisitiza umuhimu wa kuimarisha juhudi za kuwalinda Watoto dhidi ya Ukatili na hatimaye kuvitokomeza kabisa.
Kwa kutumia siku hii wananchi wote wanahimizwa kujiandaa na kujitokeza kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi tarehe 23 Agosti, 2022 na kwamba Ushiriki wa wananchi kwenye sensa utaiwezesha Serikali kupata taarifa na takwimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Taifa.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Stanslaus Nyongo ,amesema kwa sasa malezi ya watoto yanahitaji msukumo tofauti na malezi ya miaka ya nyuma kwa sababu Dunia imebadilika.
“Mhe Mgeni Rasmi na ndugu waalikwa Naomba nimuhakikishie Mgeni Rasmi na wananchi wote kuwa nikiwa Mwenyekiti wa Kamati pamoja na wanakamati wenzangu tutasimama kidete kutetea Ajenda yoyote inayohusu kupinga ukatili ndani ya Jamii ikiwemo kuishauri na kuisimamia Serikali katika usimamizi wa sheria zinazowalinda watoto” amesisitiza Mhe. Nyongo.
Naye Mbunge wa Nachingwea, Mama Salma Kikwete akizungumza katika maadhimisho hayo amewaasa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kuruhusu Mtoto ashiriki mabaraza na klabu za watoto shuleni kwani inajenga uwezo wa mtoto katika kufikiri, kujiamini na kujieleza.
“Lazima tuhakikishe ulinzi kwa Mtoto hasa vifaa vya kielektroniki kama simu na luninga bila uangalizi wa karibu ili kumwepusha kufanyiwa ukatili wa mtandaoni pamoja na matumizi yaliyopita kiasi yanaweza kusababisha urahibu kwa mtoto, athari zake ni pamoja na kukosa muda wa kujisomea na kusaidia kazi za nyumbani,”amesema.
Pia amewataka wazazi na walezi kuwq wepesi wakutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa watoto kwenye Dawati la Jinsia na Watoto kwenye vituo vya polisi ili kupatiwa msaada ikiwa ni pamoja na kuwalekeza watoto kutimiza wajibu wao wa kuwaheshimu wazazi, walimu na wanajamii na kufanyia kazi maelekezo wanayopewa ili kuwa salama kwa ustawi na maendeleo yao.