Mbunge viti maalumu mkoa wa Mtwara ,Anastazia Wambura akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wanawake viongozi unaoendelea jijini Arusha.
………………………………………
Julieth Laizer,Arusha-Arusha.
Wanawake kutoka nchi mbalimbali za Kanda za Afrika wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi zao huku jamii ikitakiwa kutoa kipaumbele kwa wanawake hao katika kuongoza nafasi hizo.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mtwara Anastazia Wambura wakati akifungua mkutano wa wanawake viongozi wanawake unaoendelea mkoa Arusha katika makao ya jumuiya ya Africa mshariki kwa niaba ya spika wa spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ambapo amesema kuwa ni vema wanawake wakapata nafasi za uongozi kwani mwanamke ndiye mzazi,mlezi, mtu mwepesi wa kubaini matatizo katika jamii pamoja na chombo kikubwa Cha amani.
Amesema wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazozuia wao kuingia katika nyanja za siasa/uongozi ikiwemo kukabiliwa na shughuli nyingi za kifamilia hivyo katika mkutano huu watajadili changamoto hizo na namna bora ya kuweza kukabiliana nazo.
Aidha Wambura amesema kuwa,mambo mengine yanayochangia ni Mila, desturi na tamaduni ambazo zinawaona wanawake ni viumbe duni ambao hawawezi kutoa maamuzi kwahiyo mambo kama haya ndo yanaenda kujadiliwa lakini pia kubadilishana uzoefu kati ya nchi na nchi kuona wao wamewezaje kwa mfano Rwanda utaona wao wako karibia asilimia 64 ya wabunge ni wanawake lakini kwetu Tanzania ni asilimia 37 na wapo ambao wapo chini ya hapo hivyo tutabadilishana .
Kwa upande wake Waziri wa jumuiya ya Africa mashariki kutoka Uganda,Dk Rebecca Kadaga amesema kuwa amekuwa spika wa Bunge la Uganda kwa miaka kumi hivyo yupo katika mkutano huo kubadilishana uzoefu nini wafanye ili wanawake waweze kupata nafasi za uongozi ikiwemo kukagua mambo mbalimbali ya serikali ikiwemo bajeti na uwakilishi wa wanawake kwa kuhakikisha asilimia 30 wanashiriki.
“ Tunataka kuhakikisha kuwa katika maeneo yetu kunakuwa na shule sahihi kwaajili ya watoto wa kike kwahiyo tupo kushauri kuhakikisha tunapaza sauti kwa pamoja na kufikia malengo ya kidunia katika nchi zetu za kuleta usawa katika mambo mbalimbali ikiwemo nafasi za uongozi,”amesema.
Naye Katibu mkuu wa umoja wa wanawake wa Bunge la jumuiya ya Africa mshariki (EALA) Fatma Ndagiza amesema kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo ni kuwapa nafasi wanawake waliopo katika siasa nafasi na kubadishana mawazo na uzoefu hasa jinsia gani walifika katika nafasi walizonazo zinazotoa uamuzi, kuelezana changamoto na ninamna gani wataweza kuzikabili changamoto hizo.
“Tunatarajia kuwa baada ya mazungumzo haya tutakuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo ya kujitahidi kubadili Katiba za nchi zetu au kama wawakilishi tuweze kufuatilia na kuhoji serikali zetu ili wanawake wawe na mchango kwa maendeleo ya taifa zao lakini pia wawe na wanawake wengi katika ngazi za siasa,” amesema.