**********************
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ameagiza kuchukuliwa hatua wale wote wanaobainika kusababisha hasara kwenye hoja za ukaguzi wa mahesabu na kuhakikisha hoja zote ambazo hazijafungwa zifungwe ifikapo September 30 mwaka huu.
Vilevile ameagiza Halmashauri Mkoani hapo ,kuweka vipaombele ,kufungua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na Kuwa wabunifu ili kukuza uchumi na kuongeza uwezo wa Halmashauri .
Akizungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Kibaha , wakati wa Kikao Maalumu cha Kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,Kunenge aliwaasa watendaji kujenga tabia ya kuhifadhi na kutunza nyaraka ili kuepusha hoja ambazo zipo ndani ya uwezo wa kuzifunga.
“Utaratibu wa ukaguzi unafahamika kama ni nyaraka hazionekani mtapewa Muda wa kuweka mambo sawa kwanini mnasubiri kuletewa hoja za kujibu kwa maandishi? Inaonesha kuna watumishi wenye dharau ,wanaopuuzia mambo hamtoi Ushirikiano wakati wa kujibu Hoja.
Alionya kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kupuuzia mambo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha hatua za ukaguzi kukwama.
Kuhusu mabadiliko ya kiuchumi mkoa , Mkuu huyo wa mkoa alisema ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kasi za ufanyaji kazi ili kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi.
“Watendaji na wataalamu muwe wabunifu unaoendana na spidi ya Serikali na Rais Samia Suluhu kuleta matokeo chanya kwa wananchi,” mkoa bado unahitaji nguvu ya pamoja kuinua uchumi,'”! ambao bado kimkoa haupo vizuri kwani Hadi Sasa mkoa upo mkoa wa tatu kutoka mwisho”alifafanua Kunenge.
Kunenge aliziasa, Halmashauri hizo, kumaliza miradi yote viporo ,kuweka Mazingira Bora ya kuvutia wawekezaji pamoja na kutangaza fursa mkoa.
Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoani Pwani ,Mary Dibogo alibainisha , wanaendelea na hoja nyingine za nyuma , wanashindwa kufunga baadhi ya hoja kutokana na Kuwa hawaoni namna ya kuzifunga .
Alitoa Rai Halmashauri zote ambazo bado Kuna hoja hazijafungwa ,wafunge hoja zilizobaki kwa muda waliopewa .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mshamu Munde alieleza , Halmashauri hiyo imepata hati safi mwaka wa tatu mfululizo na kueleza hoja zilikuwa 50 ,zilizofungwa 31 ,bado 19 hazijafungwa .
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Butamo Ndalahwa alielezea wamepata hati safi ,hoja 37 zimefungwa ,” 26 hazijafungwa kati ya hizo 18 zipo nje ya uwezo wao kuzifunga.