Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga akiongea na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Mafinga Mji wakati wa baraza la kupitia hoja za CAGMkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga akiwa na mwenyekiti na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji wakati wa baraza la kupitia hoja za CAGMkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji Happiness Laizer akiongea wakati wa baraza la kupitia hoja za CAG
Na Fredy Mgunda,Iringa.
HALMASHAURI ya Mafinga Mji imepogezwa kwa kupata hati safi
miaka sita mfululizo kutoka kwa mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) ambayo
imeendelea kuupatia heshima mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa baraza za kupitia hoja za CAG,mkuu wa mkoa
wa Iringa Queen Sendinga alisema kuwa kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano
umepelekea halmashauri hiyo kupata hati safi.
Sendiga alisema kuwa baraza la halmashauri ya Mafinga Mji kwa
kufanya kazi vizuri na ndio wamekuwa mfano kwa halmashauri nyingine za mkoa wa
Iringa kuwa na uongozi bora na wenye ushirikiano.
Aliwataka watumishi wa halmashauri ya Mafinga Mji kuendelea
kufanya kazi kwa kujituma kulingana na eneo ambalo analifanyia kazi.
Sendiga alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji
kuwachukulia hatua za kisheria kwa watumishi ambao wamekuwa wazembe kazini na
kusababisha hoja za CAG.
Alisema kuwa haiwezekani kila wakati mtumishi anakuwa
anasababisha hoja za CAG na hakuchukuliwi hatua yoyote na anaendelea kufanya
kazi hapo hapo bila kuwajibishwa.
Sendiga alisema kuwa zilipatikana hoja 30 za mkaguzi wa hesabu
za Serikali (CAG) ambapo jumla ya hoja kumi na tatu (13) zimefanyiwa kazi na
hoja kumi na saba (17) bado hazijafanyiwa kazi hivyo amegiza hoja hizo
zifanyiwe kazi haraka iwezekavyo.
Aliongeza kuwa haiwezekani watumishi wawili ndio wachukuliwe
hatua za kisheria wakati wengine wakiwa wameacha bila kuchuliwa hatua hivyo
amemugiza mkurugenzi kuwachulia hatua za kisheria watumishi.
Sendiga alisema kuwa baadhi ya watumishi ambao wanahusika
kukusanya mapato wamekuwa sio waamifu kwa kuwa wamekuwa wanazima mashine za
kukusanyia mapato.
“Haiwezekani mashine inazimwa kwa zaidi ya siku 1000
haifanyi kazi na viongozi mpo hapo haiwezekani kabisa nakwambia mkurugenzi
wachukuliwe hatua kali watumishi wanaosababisha kupotea kwa mapato ya
halmashauri”alisema Sendiga
Alimazia kwa kusema kuwa matumizi yoyote ya fedha za halmashauri
lazima yafuate utaratibu na kanuni zake ili kuhakikisha hazitokei hoja
nyingine kwa CAG.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema
kuwa Wanafanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato, ushirikiano mzuri,wanatoa
mikopo, wanafanya vizuri kwenye uchumi kutokana na kufanya kazi kwa
ushirikiano.
Mtambule alisema kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji
amekuwa kiunganishi kikubwa baina ya wakuu idara na wafanyakazi wengine wa
halmashauri kuwa kitu kimoja katika kufanya kazi.
Alisema kuwa ukatilii wa kijinsia bado upo wilaya ya
Mufindi lakini wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi
wanajua madhara ya ukatili wa kijinsia na kupinga vitendo vyote ya ukatili.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji Happiness
Laizer alisema kuwa wameyapokea maagizo yote ya mkuu wa mkoa wa Iringa Queen
Sendinga juu ya hoja za CAG na watayafanyia kazi ili kuhakikisha hawapati hoja
nyingine mpya huku wakijitahidi kuzijibu na kuzimaliza hoja zote za CAG.