*****************************
NJOMBE
Wakati TANESCO ikitambulisha mfumo wa Kidigiti wa Ni-Konekt wa kuwaunganishia huduma ya umeme wateja wapya ,Serikali ya mkoa wa Njombe Imelitaka shirika hilo la Umma kuandaa timu ya watalaamu wa kompyuta watakaokuwa tayari muda wote kukabiliana na wimbi la wadukuzi wa mifumo(HUCKERS) wanasumbua dunia ambao wanaweza kuingilia mifumo na kusababisha hasara na taifa kuwa gizani kwa muda.
Kindamba anasema mfumo huo mpya unapunguza usumbufu,Utapeli na muda ambao ulikuwa unatumika kufata taratibu za kuanganishwa umeme.
Awali meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini Mhandisi Sotco Nombo na meneja wa shirika la umeme TANESCO mkoa wa Njombe mhandisi Endrew Lukasi wanasema tayari shirika linatoa elimu ya matumizi ya mfumo huo kwa wananchi na kupata matokeo chanya na kisha kuweka bayana namna walivyojipanga na wadukuzi wa mifumo mtandaoni.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Jonisia Mgaya na Gerard Abdallah wametoa hisia zao kuhusu mfumo huo wa kidijitali ambapo wamesema utapunguza ruswa na utapeli kwa wateja.