Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2022/23, bungeni, jijini Dodoma.
……………………………….
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akisoma Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2022-2023 iliyosomwa Bungeni jijini Dodoma.
Dk.Mwigulu amesema ili kufikia azma hiyo wataanza kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania kuanzia umri wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au zaidi kujisajili.
“Napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi,”amesema
Aidha amefafanua kuwa kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao.