NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
KAIMU
KATIBU TAWALA anayeshughulikia masuala ya Rasilimali Watu Mkoani Morogoro, Bw.
Herman Tesha amewaasa Maafisa Utumishi na Utawala nchini kuwasaidia wafanyakazi
katika mchakato wa kutaarifu na kupata stahiki zao kwenye Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) pindi wanapopatwa na changamoto za kuumia, kuugua au kufariki
kutokana na kazi.
Aliyasema
hayo wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uelewa Maafisa hao kuhusu Huduma za
WCF na masuala ya Usalama na Afya Mahali pa kazi mkoani Morogoro, hivi
karibuni.
“Najua
mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya ambayo hamkuwa nayo hapo awali, mimi
binafsi nimeshawahi kuhudhuria mafunzo kama haya na nimefaidika sana, nitoe rai
kwenu nyote mtumie elimu mliyoipata kuwasaidia wafanyakazi wenu kupata stahiki
zao pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi, na kwa kufanya
hivyo mtakuwa mmeusaidia Mfuko kutimiza lengo la kuanzishwa kwake. ”
Alisisitiza na kutoa mfano… Mimi mwenyewe ofisini kwangu, watumishi wetu watatu
wamefaidika na Mfuko huu tena bahati mbaya zaidi mmoja alifariki lakini ukweli
wategemezi wake wanaendelea kufaidika na WCF.” Alisema
Kwa
upande wao washiriki wamefurahishwa na elimu waliyoipata kwani wameahidi
kupitia mafunzo hayo kila mmoja ataenda kutenda kwa usahihi kwa mujibu wa
sheria na miongozo.
“Huduma
ya Mtandao ninafahamu ni kitu kizuri sana kwa sisi waajiri kwani tunaweza
kuingia kwenye mtandao na kutoa taarifa kwa wakati na mtumishi ataweza kupata
stahiki yake kwa wakati.” Alisema Bi. Leila Komba, Afisa Utumishi Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha
Wameushukuru Mfuko kwa kutoa mafunzo hayo na wangependa yawe endelevu.
“Sisi
tuliobahatika kupata mafunzo haya basi tukawafundishe wenzetu wakiwemo waajiri
wetu.” Alisema mshiriki mwingine Bi. Leticia Machibya kutoka Ofisi ya Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Awali
akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Mkurugenzi wa
Huduma za Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulssalaam Omar, alisema hilo ni kundi
la kwanza la Maafisa Utumishi na Utawala au Maafisa Rasilimali Watu kutoka
katika taasisi za Umma kupata mafunzo hayo.
“Tulianza
kutoa elimu kama hiyo kwa Maafisa Utumishi kutoka katika Halmashauri”. Akifafanua
Dkt. Omar.
“Tunafahamu
kuwa Maafisa Utumishi na Utawala ni kiungo muhimu sana katika kazi zetu kama
Mfuko wa Fidia, kwa sababu wafanyakazi wanapopata changamoto hatua ya kwanza
wanawataarifu ninyi na nyie mnao wajibu wa kumtaarifu Mkurugenzi Mkuu kwa niaba
ya waajiri wenu, hivyo tumeona ni muhimu kwenu kupata elimu zaidi.”
Alisisitiza.
Mafunzo
hayo yalihusu uelewa wa jumla kuhusu WCF, Mafao ya Fidia yanayotolewa na Mfuko
na Jinsi ya kutoa taarifa za matukio endapo mfanyakazi ataumia, kuugua au
kufariki kutokana na kazi kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa Mada kuhusu Mafao yanayotolewa na Mfuko
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na Maafisa Utumishi na Maafia Utawala kutoka taasisi za Umma.
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Rasilimali Watu na Utawala Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Tesha
Baadhi ya Maafisa Utumishi na Maafia Utawala kutoka taasisi za Umma, wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Afisa Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi WCF, Bw. Robert Duguza, akifuatilia mijadala kwenye makundi.
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani Morogoro, Bw. Athumani Khalfan, akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia.
Mshiriki wa mafunzo, Bi. Leticia Machibya, akizungumza kwa niaba ya wenzake.
Mshiriki akionyesha jinsi alivyoweza kupata ukurasa wenye maelekezo ya kutoa taarifa kwa njia ya mtandao kupitia WCF Portal
Bi. Tumaini Kyando kutoka WCF, akifuatilia mjadala kwenye makundi
Majadiliano ya vikundi.