Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael akimsikiliza Msanii wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Jim lyke akizungumza kuhusu filamu anayotarajia kuifanya wakati wa kikao kilichofanyika leo ofisini kwake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael (kulia) akisisitiza kwa Msanii wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Jim lyke (katikati) kutangaza vivutio vya Tanzania kupitia filamu wakati wa kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Wonderland Africa, Said Rukemo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael (kulia) akikabidhi zawadi ya t-shirt yenye nembo ya Ngorongoro kwa Msanii wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Jim lyke baada ya kufanya mazungumzo kuhusu kutangaza vivutio kupitia filamu katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael (kulia) akikabidhi zawadi ya diary kwa Msanii wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Jim lyke baada ya kufanya mazungumzo kuhusu kutangaza vivutio kupitia filamu katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake jijini Dodoma.
****************************
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael amekutana na kufanya mazungumzo na Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria, James Ikechukwu maarufu kama Jim lyke na kukubaliana kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kupitia filamu.
Kikao hicho kimefanyika leo Juni 15, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii za Swagaswaga jijini Dodoma.
“Ninakupa fursa ya kutumia hifadhi zetu unapotengeneza filamu yako ili kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania” Dkt. Michael amesisitiza.
Aidha, amemtaka msanii huyo kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini akitolea mfano wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni Hifadhi Bora katika Bara la Afrika, ili ajionee Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii.
Naye, Msanii Jim lyke amemshukuru Katibu Mkuu, Dkt. Michael kwa kumpatia fursa hiyo na kusema kuwa anatarajia kutengeneza filamu itakayoshirikisha wasanii wa hapa nchini na kwamba atahakikisha anatumia zaidi vivutio vinavyoongoza na kutambulika zaidi duniani.