Na Silvia Mchuruza-Bukoba, Kagera.
Watu wenye ualibino wameiomba serikali kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili vinavyojitokeza katika jamii ili kuwalinda zaidi watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hayo yamebainishwa katika lisala iliyosomwa Bi Christmas Silas ambae ni afisa huduma chama Cha watu wenye ualbino Tanzania katika kilele Cha maadhimisho ya Siku ya uelewa kuhusu ualbino kitaifa yaliyofanyika mkoani kagera ambapo kauli mbiu ilisema takwimu kwa afua tujitokeze kuhesabiwa sensa 2022 ikiwa Ni maadhimisho ya 17 kitaifa na ya 8 kimataifa.
Nae mkuu wa mkoa wa kagera ambae alikuwaga mgeni rasmi kwa niaba ya waziri wa tamisemi mh. Innocent Bashungwa Meja Jeneral Charles Mbuge amesema serikali itaendelea kuhakikisha inapambana na changamoto kubwa zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini.
Rc mbuge amesema serikali imeweza kuimalisha upatikanaji wa elimu kwa Watoto wenye ulemavu ambapo kwa mwaka huu 2022 jumla ya Watoto 2,883 wameandikishwa kwenye elimu ya awali wakiwepo wasichana 1413na wavulana 1470 kwa ngazi ya msingi jumla ya Watoto 3518 wakiwemo wasichana 1862 na wavulana 1656 na kwa ngazi ya sekondali jumla ya Watoto 1157 wakiwemo wasichana 562 na wavulana 593.
Pia Rc mbuge ameongeza kuwa bado serikali inaendelea kutatua changamoto zinazopatikana wakabili watu wenye ulemavu wa ualbino kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwani kwa Hadi kufikia January idadi ya wanafunzi wenye ualbino kwa ngazi ya awali na msingi imefikia idadi ya wanafunzi 2564 wakiwemo wasichana 1246 na wavulana 1318 upande wa Sekondali jumla ya Watoto wenye ualbino wapatao 755 wakiwemo wasichana 383 na wavulana 372 na kwa upande wa kubaini Watoto wenye ualibino kwa ajili ya memkwa jumla ya Watoto 122 wamesajiliwa Hadi kufikia June mwaka huu.
Na kujengwa kwa miundombinu ya mabwaeni katika shule za msingi zilizo katika halmashauri 56 nchi lengo likiwa kuwawezesha wanafunzi hawa kusoma pasipo kuwepo na bugudha yoyote katika masomo yao.