Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma, Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) wakifurahia jambo baada ya kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma, kabla ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto), wakifuatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) baada ya kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Lawrance Mafuru, baada ya kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiteta jambo na Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo (kushoto) na Bi. Amina Khamis Shaaban (katikati) katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)