Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Singa Kata ya Kinampundu katika ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) aliyoifanya hivi karibuni wilayani Mkalama.
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singa katika ziara hiyo.
Wananchi wakijiji cha Singa
wakicheza ngoma wakati wakimkaribisha Mkuu wa wilaya katika ziara hiyo.
wa CCM Wilaya ya Mkalama Lameck Itungi akizungumza katika ziara hiyo.
Wananchi wa kijiji cha Singa wakiwa kwenye mkutano wa mkuu
wa mkoa .
Katibu tawala wa Wilaya ya Mkalama,.Elizabeth Rwegasira
akifanya utambulisha kwa watumishi wa Halmashauri pamoja na msafara uliongozana
na Mkuu wa Mkoa wa Singida.
kutoka ngazi ya wilaya na Mkoa
wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa katika kijiji cha Mnguli kitongoji cha Kipamba.
wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gumanga, James Mkwega akitoa neno la shukrani kwa serikali ya awamu ya sita kwakutoa fedha za utekelezaji wa miradi kwa
wilaya ya Mkalama ambapo pia
amesema wataunga mkono juhudi za serikali
kwa kusimamia fedha za miradi vizuri pamoja na kufanya kazi kwa
bidii kwa masilahi mapana ya wilaya na wananchi wa Mkalama.
Diwani wa Kata ya Mwangeza ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkalama, Bosco Samwel akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha
Munguli Kitongoji cha Kipamba wakitumbuiza kwa ngoma za asili za jamii ya Wahadzabe wakati wa ziara ya Mkuu
wa Mkoa katika Kijiji cha Munguli.
ukiendelea.
Afisa Mazingira Wilaya ya Mkalama, Amon Sanga akieleza utekelezaji wa mradi wakurejesha
Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unaotekelezwa katika Kata ya
Mpambala kwa vijiji vya Nyahaa, Mkiko, Mpambala , Lugongo pamoja na Kata ya
Mwangeza Kijiji cha Munguli.
wa TASAF Wilaya ya Mkalama, Gudluck Mlau akieleza namna mradi wa kunusuru
kaya masikini unavyotekelezwa
wilayani humo.
Mratibu wa Sensa Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha akieleza maandalizi ya sensa ya watu
na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti
23 mwaka huu.
Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe Edward Mashimba akitoa
neno la shukrani kwa ujio wa Mkuu wa Mkoa katika Kitongoji cha Kipamba ambapo
alisema jamii ya Wahadzabe iko tayari kushiki shughuli zote zamaendeleo pamoja na kushiriki katika zoezi la sensa ya
watu na makazi ifikapo Agost 23 mwaka
huu.
Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Mahenge akiwa katika
picha ya pamoja na wananchi wa jamii ya wahadzabe pamoja na wataalamu
mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Rachel Joram na Dotto Mwaibale, Mkalama
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt . Binilith mahenge ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutenga kiasi cha sh.2,118,079,899.00 kutoka kwenye mfuko wa kimataifa wa mazingira katika
kutekeleza mradi wa kurejesha Ardhi
iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula
katika kata ya Mpambala na Kata ya Mwangeza Kijiji cha Munguli Wilaya
ya Mkalama mkoani Singida
Dkt. Mahenge aliyasema hayo katika
ziara aliyoifanya wilayani hapa ya kutembelea miradi mbalimbali
ya maendeleo inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF) katika Kijiji cha Singa Kata ya Kinampundu na Kijiji cha Munguli Kitongoji cha Kipamba Kata ya Mwangeza na kusema kukamilika kwa mradi hiyo itatatua changamoto
nyingi za wananchi ikiwani pamoja na
kutatua kero za maji, na kutunza mazingira , kuzuia mmomonyoko kwenye maeneo
yanayotekelezwa miradi.
Aidha amewataka wataalamu wa ngazi zote kusimamia vizuri
pamoja kushirikiana kutatua changamoto
zitakazojitokeza ili kuharakisha maendeleo ya Wananchi wa wilaya ya mkalama ikiwa ni pamoja
na kutatua migogoro mbalimbali iliyopo katika maeneo ya miradi.
Akitembelea bwawa la kijiji cha Singa kata ya Kinampundu liliochimbwa na wanufaika wa mradi wa kunusuru
kaya masikini TASAF aliwataka wananchi hao kutumia mradi huo vizuri ili uweze
kuwanufaisha kwakuwataka kulima kilimo cha umwagiliaji na kutoruhusu mifugo
kuingia na kukanyaga kujaza mchanga kwenye mradi ili maji hayo yaweze kudumu hadi kipindi cha masika.
Awali akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alianza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa
kutembelea wilaya ya mkalama kujionea
maendeleo ya wilaya na kuongeza kuwa ziara yake inachochea kasi ya maendeleo kwani
wananchi wanajisikia furaha kutembelewa na viongozi wa kubwa huku akimuomba
Mkuu wa mkoa Dkt . Mahenge inapotokea
kugawanywa maeneo ya utawala na Kata ya Mwangeza iangaliwe kwa jicho la pekee
kwani ni kubwa hivyo kupunguza ufanisi wa kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya
mbali.
Diwani wa Kata ya Mwangeza Bosco Samwel
aliongeza kuwa ni kweli Serikali imefanya mambo makubwa katika kata yake
na hasa kwa jamii ya Wahadzabe inayoishi
kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba lakini kilio
bado kipo kwenye ubovu wa miundo mbinu ya barabara , umeme, ukosefu
wa nyumba za walimu pamoja na uhaba wawalimu
katika shule shikizi ya Kipamba ambayo tayari imesajiliwa pamoja na shule
shikizi ya Mwasulagi ambayo hakuna barabara ya kufika katika shule hiyo.
Afisa Mazingira Wilaya ya Mkalama Amon Sanga alieleza
utekelezaji wa mradi wa mazingira umesaidia kuwepo kwa mpango wa matumizi bora
ya ardhi kwa vijiji vitano
vinavyotekeleza mradi wa LDFS ,huku vikundi vya uzalishaji kiuchumi vikianza
kunufaika na ufugaji kwa kupata mizinga ya nyuki 420 pamoja na kuwepo kwa msitu ambao tayari
una hati miliki ya kimila unaotoa manufaa
mbalimbali ikiwa ni pamoja na
ufugaji wa nyuki, upatikanaji wa mahitaji ya
jamii ya kihadzabe kama vile dawa,mizizi , matunda na wanyama pori.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa TASAF Mratibu wa TASAF Wilaya ya Mkalma, Gudluck Mlau alisema kuwa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi
Mei 2022 Halmashauri ya Wilaya ya
Mkalama im epokea kiasi cha Tsh,.1,591,881,600.00 na malipo yamefanyika katika
vijiji vyote 70 ambapo jumla ya walengwa 7,235 walinufaika na mradi huo huku
kijiji cha Munguli kikipokea fedha za
ruzuku kiasi cha Tsh.43,998,000.00 kwa
kipindi cha mwezi Januari hadi Mei 2022 huku walengwa 354 wakipokea
ruzuku zao kwa njia ya mtandao jambo linalowapa urahisi wakupokea fedha zao .
Sanjari na hayo Mratibu
wa Sensa Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha
alieleza maandalizi ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika
Agosti 23 mwaka huu kuwa yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa tayari
hamasa imeshafanyika kwa vijiji vyote70 vya wilaya ya Mkalama na tayari
eneo Maalumu limetengwa katika kitongoji
cha Kipamba kijiji cha Munguli maalumu
kwa jamii ya wahadzabe na bajeti maalumu
imewasilishwa ofisi ya Takwimu taifa
ili jamii hiyo iweze kupata chakula katika siku hiyo ya sensa na kuweza
kushiriki kikamilifu.
Baadhi ya wananchi wajamii ya wahadzabe wameishukuru
serikali kuweka kipaumbele na kupeleka miradi mingi katika jamii hiyo huku
wakiaahidi kuunga mkono juhudi za
serikali kwa kufanya kazi kwa bidii na kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ifikapo Agosti 23 mwaka huu.