Na Silvia Mchuruza,Bukoba, Kagera
Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa kagera imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kupitia mh. Rais samia Suluhu Hassan kwa kutoa kauli ya kusamehewa Kodi kwa wafanyabiashara wa mkoa wa kagera iliyokuwa imerimbikizwa kwa kipindi Cha nyuma.
Pongezi hizo zimekuja baada ya ziara ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan ya siku tatu mkoani kagera ambapo alihutubia taifa kupitia mkoa wa kagera na kutoa msamaha wa Kodi kwa wafanyabiashara biashara iliyokuwa imerimbikizwa kwa mda mrefu kipindi Cha nyuma.
Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa kagera ndg.Nicholaus Jovin amesema kutolewa kwa kauli hiyo kumechochea muitikio kwa wafanyabiashara kufanya biashara pasipo wasiwasi kwani kipindi Cha nyuma wafanyabiashara walikuwa wanakumbana na changamoto nyingi.
Aidha ameongeza kuwa licha kusamehewa Kodi pia imefunguliwa mipaka kwa ajili ya wafanyabiashara wa mkoa wa kagera na hata nje ya mkoa kwa kufuata kanununi na sheria zilizowekwa na kusema kuwa pia Jumuiya inampongeza mh. Rais kwa kuwaletea tawi la chuo kikuu Cha dar es salaam katika mkoa kwana nacho ni chanzo Cha kukuza uchumi wa mkoa wa kagera .
Hata hivyo nao wajumbe wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa kagaera akiwemo ndg. Richard Maganga amesema kuwa uchumi wa mkoa wa kagera unawategemea wanakagera wenyewe wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia ameongeza kuwa Jumuiya inampongeza mh rais kwa kuendelea kuwaondolea vikwazo na kuwapatia msamaha wa Kodi za malimbikizo za kipindi Cha nyuma kwani kabla ya msamaha huo Jumuiya ilikuwa inapitia changamoto nyingi.