Mjumbe wa Kamati ya Uratibu ya Programu ya Kukuza Ujuzi (ESP) kutoka wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Margaret Mussai,akizungumza wakati akifungua Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
Meneja Programu wa ESP kutoka CIcan-Canada, Tom Tunney,akielezea namna programu itakavyosaidia wakati wa Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
MWAKILISHI Masuala na Ushirikiano wa Kimataifa Canada,Stephen Kijazi,akizungumza wakati wa Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
MENEJA na Mshauri Mkuu wa Programu Dkt.Alan Copeland,,akizungumza wakati wa Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma.
Mshauri Mkuu wa Masuala ya Jinsia (STA)Dkt.Alice Mumbi,akizungumza wakati wa Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
Mjumbe wa Kamati ya Uratibu ya Programu ya Kukuza Ujuzi (ESP) kutoka wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Margaret Mussai,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Warsha ya Siku 4 kwa Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs),Asasi za Kijamii (CBOs),Maafisa Maendeleo ya Jamii(CDOš), na MoEST / DTVÉT kilichoanza leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma
……………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kwa kushirikaina na Umoja wa Taasisi na Vyuo vya Canada (Canada-CICan) wameandaa Programu ya kukuza ujuzi wa kujiajiri(ESP) kwa wasichana waliokatisha masomo.
Progarmu hiyo itafanyika kwa miaka saba nchini (2021-2028) na inatekelezwa na Umoja wa Taasisi na Vyuo Canada(Canada-CICan) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Idara ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (DTVET).
Akifungua Warsha ya Wadau wa ESP wakiwamo Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDCs) leo Juni 13,2022 Jijini Dodoma Mjumbe wa Kamati ya Uratibu ya Programu ya Kukuza Ujuzi (ESP) kutoka wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Margaret Mussai amesema Programu hiyo imewekeza kiasi cha Shilingi bilioni 45.4 zitakazotumika kuzijengea uwezo FDC 12 na CBO 12 katika maeneo mbalimbali
Pia itachangia na kuimarisha maeneo ya elimu ya kujiajiri na kuajiriwa, ujasiriamali kwa wasichana na wanawake.
Aidha, kwa kufanya kazi na FDC na CBOs katiak FDC 12, programu hii inadhamiria kuongeza kiwango cha ushiriki wa wasichana na wanawake katika mafunzo ya kukuza ujuzi na biashara, jinsia na haki za binadamu katika jamii.
“Programu hii ni muhimu sana kwa taifa letu kwani itatusaidia Kuandaa na kutoa mafunzo ya ujuzi ya muda mfupi, walengwa wakuu wakiwa ni wasichana na wanawake720. Aidha, kupitia CBOs wanawake 480 katika jamii watafikiwa na kupata elimu hiyo,Kutoa mafunzo ya Jinsia na haki za binadamu kwa walimu na watumishi 180 kati yao wanawake 60 na wanafunzi 3,200 (Ke 1,000)”Amesema Mussai
“Kuzishirikisha jamii katika shughuli za uhamasishaji na uelimishaji kutambua faida za msichana kujiendeleza kimasomo na kumpa nafasi mwanamke kushiriki mafunzo ya kujenga na kukuza ujuzi ili kujikomboa kiuchumi Wanajamii 2,400 (Ke 1,200) na wanachi watakaojitolea (Volunteers) 36(Ke24) watanufaika na mafunzo haya,”
Mussai amesema kuwa Matokeo mazuri ya Programu hii yatatoa fursa kuwa na mikutano itakayowezesha kubadilishana uzoefu kwa kile jamii ilichojifunza na kupanua wigo kwani Washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi watakutanishwa kuelimishana matokeo na faida ya utekelezaji wa programu ili kuchukuwa yale yenye manufaa na kwenda kuingiza katika afua zao.
Aidha ameahidi kuwa Wizara hiyo itasimamia kikamilifu utekelezaji na kuhakikisha malengo ya program ya kukuza ujuzi yanafikiwa na vijana wa Tanzania.
Kwa upande wake Meneja Programu wa ESP kutoka CIcan-Canada, Tom Tunney, amesema kuwa anaamini ushirikiano unaoletwa na ESP utakuwa na matokeo chanya katika masuala ya usawa.
Bw.Tunney amesema kuwa katika warsha hiyo ya siku nne inalenga kujenga mtandao wa kudumu ambao dumu hata baada ya mradi kuisha, kuanza mchakato wa kuunda timu jumuishi na shirikishi za jinsia, kufanya tathmini ya mahitaji na uwezo wa utoaji mafunzo kwa asasi zinazoshiriki.
‘Programu hii inatoa fursa muhimu kwa Muungano wa Vyuo na Taasisi Canada (CICan) – na taasisi wanachama kuimarisha zaidi ushirikiano wa kitaifa na kimataifa katika maeneo muhimu ya elimu, usawa wa kijinsia, haki za binadamu, mazingira, na ukuaji wa uchumi ambao unahusu kila mtu
” Nchini Canada, utaalamu wa wanachama wetu unachangia kupunguza
umaskini na ukosefu wa usawa, hasa kwa wanawake, vijana na watu wasiojiweza, kwa
kubadilisha mifumo ya elimu baada ya kumaliza sekondari na kutoa mafunzo yanayolenga
ajira”,Amesema Tunney