***********************
Mwenge wa Uhuru leo jumapili tarehe 12.6.2022 umepitisha miradi yote yenye thamani ya jumla ya sh.Bil 1.16 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu ,mapato ya ndani ya Halmashauri na wananchi iliyotembelewa na kuwekwa mawe ya msingi na kufunguliwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa jimbo la Siha na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godwin Molel akipokea mwenge huo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kusogeza huduma za afya kwa wannchi na kuwapunguzia usumbufu kutokana na awali kwenda umbali mrefu kutafuta huduma.
“Kwa kweli Serikali tunaishukuru sana kwa huduma mbali mballi muhimu zilizosogezwa karibu ikiwemo za afya , kwani wananchi walikuwa wanapata shida “amesema Dkt. Molel.
Mwenge huo wa Uhuru mapema ulipokelewa katika wilayani na kupelekwa katika kijiji cha Lawate na baadaye kutembelea mradi wa Vijana Sanya Juu na kitalu cha Miti cha West Kilimanjaro.
Hata hivyo miradi iliyowekwa jiwe la msingi ni ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Mwangaza,ujenzi wa barabara ya Lami kwa DC-MAGADINI -KARANSI na mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Olkolili Tarafa ya Siha Kusini.
Aidha,Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Siha umefungua shule mpya ya Neema iliyopo kata ya Gararagua.
Jumla ya Miradi mitatu imewekwa jiwe la Msingi,Miradi miwili miwili ikitembelewa na mradi mmoja umezinduliwa.