**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia ndaki ya Insia imekuwa bega kwa bega kuhakikisha inatenga fedha kwaajili ya Tamsha la Taaluma na Vipaji (Sanaa Blast Festiival) ambapo mwaka jana Ndaki ilitenga Milioni 15 na imefanya hivyo mwaka huu.
Ameyasema hayo leo Juni 10,2022 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Prof.Bernadeta Killian wakati akifungua rasmi Tamsha la Taaluma na Vipaji (Sanaa Blast Festiival) lililofanyika katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam katika kusheherekea miaka 60 ya Chuo hicho.
Amesema kumekuwa na ongezeko la wasanii wanafunzi ambapo mwaka jana walikuwa 100 na hadi kufikia mwaka huu wasanii wanafunzi wameongezeka na kufikia 300 katika fani mbalimbali.
“Kumekuwa na ongezeko la wadhamini kutoka mdhamini mmoja ambaye ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Ndaki ya Insia mpaka wadhamini wanne zaidi ambao ni Hugo Domingo-wadhamini pacha, BASATA, BODI YA FILAMU, Heritage Drinking Water na Active Motion”. Amesema Prof.Killian