Mkurugenzi Mkuu wa Yoonek Cargo Tanzania Bw.Patric Barnabas (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam wakati wakitambulisha huduma yao mpya ya usafiriishaji wa mizigo kutoka nchini China kwa njia ya Maji kuja Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa Yoonek Cargo Tanzania Bw.Patric Barnabas akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam wakati wakitambulisha huduma yao mpya ya usafiriishaji wa mizigo kutoka nchini China kwa njia ya Maji kuja Tanzania
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Usafirishaji wa Mizigo kutoka China kuja Tanzania Yoonek Cargo Tanzania leo imetangaza huduma yao mpya ya usafirishaji kwa njia ya maji ambapo mizigo mingi kupitia wao wataweza kusafirisha kutoka nje ya nchi kwa kutumia meli ambapo zamani walikuwa wanatumia usafiri wa anga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Yoonek Cargo Tanzania Bw.Patric Barnabas amesema kutokana na wateja wao kwa wingi wamekuwa wakihitajji huduma ya usafirishaji wa mizigo yao kwa njia ya maji hivyo wakati kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha huduma hiyo.
“Licha ya takwa hili kutoka kwa wateja wetu, Kampuni yetu ilikuwa na lengo la ndani ya miaka mitatu iwe na uwezo na ufanisi wa kutosha ili iweze kuongeza huduma hii mpya ya usafirishaji kwa njia ya maji”. Amesema Bw.Barnabas.
Amesema kupitia huduma hiyo mpya wanatoa huduma kama vile Full Container Loads (FCL), Loose/Less than Container Loads, Group page, Consolidation na Documentation.
Pamoja na hayo amesema licha ya kuzindua huduma mpya ya usafirishaji wataendelea pia kutoa huduma yake ya usafiri kwa njia ya anga kwa haraka na ufanisi kama ilivyokuwa toka awali.