Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama cha Mapinduzi (UWT) Gaudencia Kabaka amewataka watu wanaosema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa ameupiga
mwingi waende mabli zaidi na kutaja yale mengi mazuri aliyofanya
badala ya kuishia na neno hilo.
Alitoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza wa
Jumuya ya wanawake kutoka wilaya tisa za kichama kutoka katika mkoa wa
Tanga.
“Tunae mama. Tumempa sifa nyingi. Mama mbunifu, mama mchapa
kazi.Tusiseme tu unaupiga mwingi tu… Mimi Kiswahili hicho
sikipendi.. Anaupigaje mwingi katika kata yako Kuna vituo vya afya
vimejengwa, madarasa madaraja yamejengwa. Unatakiwa kuelezea hayo.”
Amesema.
kabaka alionya kuwa kama wanawake hawatakuwa mstari wa mbele kumuenzi
Rais Samia katika uchaguzi ujao basi watanzania, hasa wanawake wasahau
kuwa na Rais mwanamke. Aliwataka kuwa na upendo na umoja na kuua kuwa
kila wanachofanya wanamtengezea Mama Samia kwa kutaja kazi anazofanya.
Aliwataka viongozi wanawake wasilale wakijfikiri mamo yanakwenda hivhi
hivi bali wanatakiwa kumsemea mambo mazuri anayofanya
Pia alisisitiza kuhakikisha jumuia inakuwa na miradi sambamba na wagombea watakaogombea wawe na vitega uchumi ili wasiwe mizigo Kwa jumuia hiyo.
Akizungumzia kuhusu Bomba la mafuta aliwataka wakinamama kutuia fursa
ambazo zinaletwa na mradi huo kujiinua kiuchumi.
Wakati huo huo, katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Sulemani Mzee ameiomba
serikali kuupa ngu ya kitaifa kukabiliana na uvamizi wa tembo katika
maeneo ambayo yanapakana na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ili kuokoa
wakazi wa maeneo hayo na adha hiyo.
Amesema hali ilivyo hivi inaonekana aaskari walioletwa katika enep
hilo wameshindwa.
Akijibu hoja hiyo., Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana
ambaye alipita katika kikao hicho kusalimia wakati akielekea kijiji cha
msomella, sehemu ambayo wahamiaji kutoka Ngorongoro wanajengewa
makazi, alisema serikali imeandaa mkakati wa kudhibiti tembo wa
kitaifa unaandaliwa.
Amesema kuwa namba ya simu maalum itatolewa kwa ajili ya kutoa taarfa
za uvamizi wa tembo ili serikali iweze kuchukua hatua kuzuia wanyama
hao wasidhuru watu na kuharibu mazao yao.