Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James (kulia) akikabidhi makusanyo kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Umoja wa Wababa Kanisa la Anglicana Achidikonari ya Ubungo (UBAKI) Moses Manyatta (kushoto) yaliyokusanywa kutoka kwa washarika na waumini wa kanisa hilo (hawamo pichani) wakati wa sherehe za kuzindua rasmi Umoja huo zilizofanyika leo Juni 11,2022 katika kanisa la Mtakatifu Batolomayo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
MKUU
wa wilaya ya Ubungo Heri James amewataka viongozi wa Dini nchini
kutumia nafasi zao kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa kwani kufanya
hivyo kunatoa fursa kwa serikali kuwafikia wananchi wake kimaendeleo.
Amesema
mwaka huu Agosti 23 ni mwaka wa sensa hivyo ni vema viongozi
wakahamasisha wananchi wao na kuwakumbusha umuhimu wa kuhesabiwa
ukizingatia zoezi hilo linafanyika kila baada ya miaka kumi.
James
Ametoa kauli hiyo leo juni 11 mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi
wa umoja wa Chama cha wababa (UBAK) wa Kanisa la Angalikana
Archidikonary ya Ubungo uliofanyika katika la mtakatifu barthromayo
wilayani humo.
“Kwanza
nawapongeza kwa uzinduzi huu wa Chama cha wababa kwani kimekuja wakati
sahihi ukizingatia mara zote tumekuwa na mambo ya akina mama tu hivyo
Chama hiki ni sehemu ya juu kwa wababa katika kuwasilisha na kutoa maoni
yao. Lakini pia tutumia umoja huu kukumbushana juu ya kulinda maadili
yetu na malezi kwa vijana wetu.”amesema.
Nakuongeza kuwa
“Serikali hususani Wilaya yangu ya Ubungo tuna mashirikiano mazuri na
Kanisa la Angalikana kupitia viongozi wake, ni matumaini yangu hata
katika hili la UBAKI tutaendelea kushirikiana pasipo shaka.
Pia
amewahamisha waumini hao kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo
wilayani humo hususani mikopo ambayo inatolewa bila riba kupitia
halmashauri ya Ubungo,nakwamba wilaya hiyo ndio lango kuu la kuingilia
mjini kati na hata stendi ya Magufuli ipo ubungo hivyo ni muhimu kuwa na
jicho la kutazama fursa zilizopo za kiuchumi.
“Ndungu
zangu kupitia Umoja huu tuimarishe malezi kwa vijana ,maadili ,na
tuendelee kukemea wizi,ufisadi,dhuluma,ukatili na uhujumu kwani haya
yote ni roho zisizokubarika katika jamii yetu“amesisitiza James.
kwa
upande wake Kasisi Kiongozi wa kanisa la Angalikana Dayosisi ya Dar es
Salaam Richard Kamenya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha UBAKI Moses
Manyatta wamesema pamoja na mambo mengine yote lakinin pia watatumia
umoja huo kuhamsisha waumini kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa
linalotarajia kufanyika kitaifa Agosti 23 mwaka huu.
Pia
wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea
kuutoa kwenye Taasisi za dini hivyo wao kama viongozi jukumu lao kubwa
ni kuendelea kusimamia utulivu uliopo.
katika
uzinduzi huo wa Chama cha Umoja wa Baba UBAKI mkuu wa Wilaya hiyo ya
Ubungo Heri James amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya
kutunisha ufuko wa umoja huo.
Viongozi wa UBAKI wakitambulishwa rasmi na kuwekwa wakfu kukiongoza Chama hicho katika hafla hiyo.
Kwaya ya Umoja wa wakina Mama Kanisa la Anglicana Ubungo (UMAKI) wakitumbuiza.