Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf katika Halmashauri wilaya ya sikonge Claud Nkanwa
………………………………………
Na Lucas Raphael,Tabora
Mpango wa kunusuru kaya maskini katika halmashauri ya wilayani Sikonge mkoani Tabora imewawezesha watoto 4901 kutimiza masharti ya elimu na watoto wapatao 1132 wanatimiza masharti ya afya wilayani humo ambapo wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wakiwa ni 4864.
Akizungumza juu ya mpango huo Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf katika Halmashauri wilaya ya sikonge Claud Nkanwa alisema kwamba toka kuanza kwa mpango wa kunusuru kaya masikini wamefanikiwa watoto hao kunufaika na masharti ya elimu na afya wilayani humo.
Alisema kwamba watoto hao wanapata elimu katika shule mbalimbali zilizopo katika vijiji 64 kwenye kata 20 zilizopo wilayani humo.
Mratibu huyo wa Tasaf wilayani Sikonge aliendelea kusema kwamba kutokana na muhimu wa elimu na afya wamekuwa wakisisitiza sana swala zima la wazazi kuhakikisha watoto wanapata sare za shule ikiwemo madafutari na vitabu vya kiada.
Hata hivyo alisema kwamba watoto wanaotimiza masharti ya Afya wamekuwa wakihudhuria kila wakati klini kwa ajili ya kuwapatia matibabu watoto waliochini ya miaka mitano
Alisema kwamba watoto chini ya miaka mitano wao wanapata matibabu bure bila kuchangia kitu chochote kile kutoka na sera ya afya ambao wa watoto wenye umri huo wanatibiwa bure kwenye hospital na zahanati zote nchini.
Akizungumza swala la mafanikio ya Tasaf wilayani humo Claud alisema kwa kipindi cha kuanzia julai 2021 hadi Aprili 2022 fedha zilizotolewa kwa walengwa ni bilioni 1,387,437,858 .
Alisema kwamba walengwa wa mpango huo wamekuwa wakipata maelekezo mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha fedha wanazipata zinatumika kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na familia zao.
Aidha alisema kwamba Mfuko wa Afya ya Jamii Tasaf umendelea kuwa mkombozi mkubwa kwa walengwa ambao wanakiri Tasaf imewasaidia sana kuwezesha kujenga kufunga kuku ,Mbuzi,Bata,Kondoo na Ng’mbe .
Alisema kwamba licha ya kufunga lakini pia wameweza kulima mazao mbalimbali kwa ajili ya kupata chakula kwa familia zao.