Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akiwasili na kupokelewa na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kwaajili ya kushiriki mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kwenye Mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki mara baada ya kuwasili katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla akizungumza mara baada ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel katika Taasisi ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kwenye mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza jambo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe.Tri Yogo Jatmiko katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bi.Kokushubila Kairuki akizungumza katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla akizungumza katika mkutano wa kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Bw.Nimrod Matungwa ambaye ni rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akizungumza katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya pamoja na wadau wa Afya wakiwa katika mkutano wa Kisayansi uliowakutanisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afya uliolenga kujadili namna bora ya kuimarisha mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI imepongeza uwekezaji uliofanywa na Mtandao wa Elimu ya Afya Kairuki (KHEN), kwenye sekta ya elimu ya afya kwani unachangia juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya.
Pongezi hizo zilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati wa kongamano la kisayansi lililofanyika jana kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert kairuki (HKMU), Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Amesema uwekezaji uliofanywa na Hayati Profesa Kairuki kwenye sekta ya afya ni mkubwa na wa kuigwa kwani umesaidia kupunguza msongamano kwenye hospitali za serikali.
Aidha Dkt. Mollel amewataka wasomi na wataalamu afya nchini kujikita katika tafiti zinazoendana na maendeleo ya teknolojia ili kuwa na mfumo wa afya utakaokuwa tayari kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama Uviko19.
“Janga la Uviko19 lilipokumba ulimwengu ilidhihirisha udhaifu katika sekta za afya ulimwenguni kwani janga hilo lilionekana kshamiri na kushindwa kudhibitika”. Amesema Dkt.Mollel.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki wataalamu wa chuo wameeleza umuhimu wa nchi kuimarisha utendaji wa mfumo wa afya na uthabiti katika kukabiliana na dharura za afya ya umma.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof.Yohana Mashalla amesema magonjwa ya kuambukiza yamekuwa changamoto kubwa sana kwa nchi zinazoendelea kulinganisha na zile zilizoendelea.
Amesema mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 umeonyesha ni kwa namna gani taifa linapaswa kuweka mifumo imara kujiandaa kukabiliana na majanga ya aina hiyo yatakapotokea siku za mbele.
“Iko haja ya kuimarisha mifumo yetu ya afya ili tuweze kujitayarisha kukabiliana na maradhi ya mlipuko kama COVID 19 na lazima tufahamu kuwa COVID siyo ya kwanza na wala siyo ya mwisho kuna milipuko itakuja tujiandae,” Amesema
Nae rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bw.Nimrod Matungwa amesema mkutano huo utakwenda kuwa chachu ya ufumbuzi zaidi kwa namna ambavyo wanaweza kukabiliana na janga la Covid-19 pamoja na matatizo ambayo yanatokea kwenye sekta ya Afya.