Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliasi Kwesi akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari kwa uongozi wa Halmashauri ya Ruangwa leo Jijini Dodoma
Muonekano wa Gari lililotolewa kwa ufadhili wa USAID AFYA YANGU kanda ya kusini litakalosaidia katika usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi
Kaimu Mkanga Mkuu wa Serikali, Dkt. Elius Kwesi akipokea ufunguo wa gari kutoka kwa Meneja Mradi wa USAID AFYA YANGU kanda ya Kusini Ndugu Nyantito Machota leo jijini dodoma
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Elius Kwesi akimkabidhi ufunguo wa gari kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa, Frank Chonya leo jijini dodoma katika hafla ya kukabidhi gari litakalosaidia katika usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi.
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Ruangwa Frank Chonya akiwakatika gari alilokabidhiwa kwaajili ya usimamizi wa huduma za afya katika halmashauri hiyo leo jijini Dodoma
***************************
Na. WAF – DODOMA
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Eliasi Kwesi ametoa wito kwa Viongozi wa Afya Mkoa wa Lindi kuhakikisha gari walilopatiwa chini ya ufadhili wa USAID kwa ajili ya kusaidia na kuimarisha huduma za afya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa linatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Dkt. Kwesi ametoa rai hiyo leo Jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya gari hilo kutoka kwa Meneja Mradi wa USAID AFYA YANGU Kanda ya Kusini Nyantito Machota, ambapo amesema gari hilo litasaidia kuimarisha huduma za afya katika wilaya ya Ruangwa.
Amesisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanaitunza gari hiyo, ikiwemo kuzingatia matengezo wakati yanapohitajika sambamba na kusimamia vema matumizi sahihi ya gari hilo.
“Tumewakabidhi gari hili kwa ajili ya usimamizi wa huduma za afya katika wilaya ya Ruangwa na hii ni hatua ya kwanza na tunaendelea kutafuta magari mengine ili wilaya zote nchini ziweze kuwa na magari katika kufanya usimamizi wa huduma za afya nchini”. Ameeleza Dkt. Kwesi.
Aidha, Dkt. Kwesi amewashukuru Wadau wa USAID AFYA YANGU kwa msaada huo, kwani utakwenda kusaidia uimarishaji wa huduma za afya katika halmashauri ya Ruangwa, huku akiomba wadau wingine kujitokeza katika kusaidia halmashauri nyingine.
Meneja Mradi wa USAID AFYA YANGU Kanda ya Kusini, Ndugu Nyantito Machota amesema kuwa, Halmashauri ya Ruangwa ni moja ya halmashauri 43 nchini zinazotekeleza mradi wa USAID AFYA YANGU kanda ya kusini na wamemekuwa wakifanya kazi na halmashauri hiyo kwa miaka mitano iliyopita na sasa wamepata mradi huu ili kusaidia kuimarisha huduma za afya katika halmashauri hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya, ameishukuru Wizara ya Afya chini ya Wadau wake USAID AFYA YANGU kwa ufadhili wa gari walilokabidhiwa ili kuboresha na kuimarisha huduma za afya katika halmashauri hiyo.
“Leo naimani tunakwenda kuchapa kazi idara ya afya katika halmashauri yetu kwa ufasaha kama ilivyokusudiwa na tunahaidi kuleta matokeo chanya kulingana na malengo ya wizara katika kutoa huduma kwa wananchi wa Ruangwa”. Amesema Chonya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt. Herry Kagya amesema kuwa ufadhili huo utasaidia Timu ya Usimamizi Huduma za Afya Ngazi ya Halmashauri (CHMT), kuweza kutekeleza vizuri majukumu yao kwa kusimamia utoaji huduma na ufatiliaji wa maswala yote ya afya ndani ya Halmashauri ya Ruangwa.
“Sasa ni wajibu wetu tumepata kitendea kazi hiki tukitumie ioasavyo kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi na kuleta matokeo chanya katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora.