*****************
Maafisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakisikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wadau waliofika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa, uliopo Soko Matola Jijini Mbeya, leo tarehe 9 Juni, 2022 ikiwa ni siku ya pili ya warsha ya uhamasishaji wadau kuhusu kanuni za Wamiliki Manufaa.
Warsha hiyo imewashirikisha wamiliki wa kampuni, mawakili, washauri wa masuala ya biashara na wadau wengine.