WATUMISHI wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) wakikabidhi Misaada ya vifaa tiba na vyakula kwa wodi ya watoto katika hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya nchini.
MENEJA Mahusiano wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Dodoma Mwanaharusi Shein ,akimkabidhi Msaada ya vifaa tiba na vyakula Daktari wa Watoto Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dk.Muzzna Ujudi mara baada ya watumishi wa PBZ kukabidhi Msaada.
Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) tawi la Dodoma Mohamed Masoud,akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba na vyakula kwa wodi ya watoto katika hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini.
Meneja Mahusiano wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Dodoma Mwanaharusi Shein ,akielezea jinsi walivyoamua kutoa msaada wa vifaa tiba na vyakula katika wodi ya watoto katika hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini
MUUGUZI Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Bw.Stanley Mahundo,akiipongeza Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Dodoma kwa kutoa msaada wa vifaa tiba na vyakula katika wodi ya watoto katika hospitali ya hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini
Daktari wa Watoto Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma Dk.Muzzna Ujudi,akitoa wito kwa Taasisi na mashirika mengine kuiga Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) ambayo imetoa msaada wa vifaa tiba na vyakula kwa wodi ya watoto katika hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa
……………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kuunga Mkono Juhudi za Rais Samia,Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) imetoa msaada wa vifaa tiba na vyakula kwa wodi ya watoto katika hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini.
Akikabidhi Msaada huo katika Hospitali hiyo Meneja wa Benki hiyo tawi la Dodoma Mohamed Masoud, amesema kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya nchini.
“Leo hii tumekabidhi vifaa tiba katika hospitali yetu ya rufani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni kuonyesha ushirikaiano wetu kwa jamii na kuthamini kile ambacho serikali yetu inakifanya kuboresha seka hii muhimu ya afya nchini”amesema Masoud
Amevitaja, vifaa walivyo kabidhi ni pamoja kiti mwendo kwa ajili ya wagonjwa wasioweza kutembea, mashuka na maziwa kwa ajii ya watoto ambao wazazi wao hawatoi mazaiwa ya kutosha vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 3.5.
“Leo tumekuja lakini hii haitakuwa mwisho tutaendelea kuja na kuona mahitaji yaliyopo hapa ili kuweza kuwahudumia watu mbalimbali wenye uhitaji”almesema
Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo Stanely Mahundo, ameishukuru Benki hiyo kwa msaada huo ambao umekuja wakati mwafaka na unakwenda kujibu baadhi ya changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo.
“Wito wangu kwa taasisi zingine kuiga mfano wa benki hii ili kuja kuungana na serikali yao katika kuboresha huduma za afya nchini”amesema
Aidha ameishukuru serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali katika hospitali hiyo ambapo hivi sasa wanatoa huduma za kibigwa zaidi ya 20.