Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano biashara na uwekezaji bunge la EALA , Christopher Nduwayo akizungumza na waandishi wa habari bungeni hapo leo.(Happy Lazaro)
*********************************
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha.Wabunge wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki wameziomba nchi za EAC hususani idara ya uhamiaji kufuata sheria za jumuiya hiyo inayoelekeza kuhusu suala la utoaji wa Viza hususani kwa wananchi wanachama ambao wamekuwa wakifanya biashara katika jumuiya hiyo.
Wamesema kuwa,kumekuwepo na changamoto katika nchi hizo katika idara ya uhamiaji kuendelea kutoa Viza ya siku saba badala ya kufuata utaratibu wa sheria uliopitishwa na nchi hizo kuwapa Viza ya miezi 6 kila mwananchi anayetaka kusafiri ili kupunguza usumbufu unaoendelea kujitokeza mipakani na kuwakatisha tamaa wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya kamati ya Mawasiliano Biashara na Uwekezaji bungeni , Mwenyekiti wa kamati hiyo bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki EALA , Christopher Nduwayo amesema kuwa, kuna haja ya nchi hizo kukaa na watu wa idara ya uhamiaji ili kuweza kufuatwa kwa sheria katika utoaji wa Viza.
Amesema kuwa, ipo haja kubwa ya kuangalia suala zima la utoaji wa Viza hususani kwa wananchi wanachama ambalo linaonekana kuwa ni changamoto kwa wananchi pindi wanaposafiri katika nchi hizo .
Amesema kumekuwepo na changamoto ya Maafisa uhamiaji katika maeneo ya mipaka kuendelea kutoa viza ya siku Saba wengine mwezi ambapo ni kinyume na utaratibu wa sheria iliyopitishwa na nchi hizo.
“Unakuta mwananchi anatoka Burundi anapewa viza ya siku Saba na Mwananchi huyo anaenda Tanzania kufika huko lazima atumie siku mbili za kwenda hapo anabakiza siku tano kufanya biashara kwa siku hizo hadi kurudi mpakani ni siku chache inayopelekea akifaka mpakani kulipa faini hii ni usumbufu kwa mwananchi na ni lazima.tuangalie Jambo hili ili wananchi wafurahie uwepo wa jumuiya yao”amesema .
Ameongeza kuwa,Jumuiya imeundwa kwa ajili ya kuwasaidia na kuondoa vikwazo vya kibiashara wafanyabiashara wanaozunguka katika kufanya biashara zao eneo moja la nchi hadi nyingine kupitia mipaka ya nchi za Jumuiya”. ameongeza Nduwayo.
“Mimi ni mbunge nilipita katika moja ya mpaka wakanigongea kibali cha mwezi mmoja tena baada ya kuuliza kihusiana na sheria hiyo ya miezi sita na bado katika Passipoti yangu waliniandikia kutofanya kazi popote sasa nashangaa mimi ni Mbunge na huku nakuja kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi wa Jumuiya ni vyema serikali zetu zikae na kutoa elimu ya kutosha kwa maafisa hawa wa Uhamiaji hususani katika mipaka yetu”amesema.
Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame amesema kuwa, bado kuna changamoto kwa baadhi ya mipaka katika vituo vya mipakani kutokuwa na makazi ya watumishi wakiwemo Uhamiaji TRA na Polisi ambapo inapelekea wafanyakazi wa Idara hizo kufanya shughuli zao bila ufanisi.
Amesemakuwa, kutokana na hilo ni vyema kila nchi itengeneze utaratibu wa kuwajengea nyumba au makazi yenye viwango watumishi wao kwenye vituo hivyo ili wafanye kazi kwa ubora na ufanisi mkubwa.
” katika kipaumbele alichopanga Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo alipoingia katika nafasi yake alipanga kazi yà kwanza ni kuongeza mwanachama wapya jambo ambalo amelitekeleza kwa kumpata DRC CONGO ambayo inamalizia utaratibu ili kuingia rasmi baada ya hilo kazi nyingine kubwa aliyopanga ni kuunda kamati ya biashara ya Afrika Mashariki ili kuokoa watu wa sekta binafsi”amesema.
Amefafanua kuwa, atatumia nguvu kuhakikisha kwa mwaka huu kamati hiyo inapatikana ili kupunguza tatizo la kodi mipakani pamoja na changamoto zake.