Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank , Bw.Abdallah Kirungi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangaza bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK. Mkurugenzi Mkuu wa FMJ Hardware Limited Bi.Fatina Said akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangaza bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK. Bi.Sabina Mwakasungura ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki ya Mwalimu akisoma taarifa mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wakitangaza bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank , Bw.Abdallah Kirungi akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa FMJ Hardware Limited Bi.Fatina Said mara baada ya kutangaza bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK.
******************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BENKI ya Mwalimu wameanzisha bidhaa yao mpya ya JENGA NA MWALIMU BANK ambayo inalenga kuwasaidia wafanyakazi kukopeshwa vifaa vya ujenzi ili kuweza kufikia malengo yao ya kumiliki nyumba na kuboresha makazi kwa bei nafuu.
Mkopo huo wanatoa kwa kushirikiana na wabia wao ambao ni Wasambazaji na wauzaji wakubwa wa vifaa vya ujenzi nchini kwa bei ya jumla na rejareja wanaoitwa FMJ Hardware limited.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 9,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank , Bw.Abdallah Kirungi mesema bidhaa hiyo imelenga kuboresha maisha ya watumishi na watanzania kwa ujumla ambapo ni bidhaa ya mkopo kwa vifaa vya ujenzi ambayo itaawezesha wateja kuweza kupata nyumba na kuboresha makazi yao.
Bi.Sabina Mwakasungura ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki ya Mwalimu amesema bidhaa hiyo imelenga kusaidia wafanyakazi kuunganishwa na huduma za umeme, maji na vinginevyo.
Amesema katika kuhakikisha usalama wa vifaa hivyo, Mwalimu Benki itaviwekea Bima ya kuvilinda dhidi ya uharibifu wowote katika kipindi cha usafirishaji wake hadi pale vitakapomfikia mteja popote alipo.
Aidha Bi.Sabina amesema kuwa huduma hiyo itaweza kuwafikia watanzania kwa wingi kwani mapaka sasa wamekuwa na matawi mawili yaliyopo Dar es Salaam pamoja na vituo tisa vya huduma katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha, Rukwa, Kigoma na Mtwara. Matajaio yao ni kuwa na vituo katika mikoa yote nchini ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa FMJ Hardware Limited Bi.Fatina Said amesema kampuni hiyo inamawakala karibu kila mkoa nchini hivyo kupitia bidhaa ya JENGA NA MWALIMU BANK watanzania watajipatia huduma hiyo kwa wepesi zaidi.
Pamoja na hayo Bi.Fatina ameishauri Benki hiyo kuhakikisha inawalenga pia watumishi wa sekta binafsi ili huduma hiyo iweze kukua na kuwafikia watanzania kwa wingi katika ameneo mengi.