Na Joctan Agustino-MAKAMBAKO
Mwananchi mmoja anajishughulisha na uuzaji wa nyama ya kuchoma katika mtaa wa Kibedange kata ya Kivavi halmashauri ya mji wa Makambako Mkoani Njombe Mbaraka Kadege amechomwa kisu shingoni na Ozwadi Kihombo kwa kosa la kudai shilingi elfu moja ambayo alikuwa anadaiwa baada ya kukopa nyama siku za nyuma.
Akizungumzia tukio hilo Mbaraka Kadege amesema mteja huyo alifika katika eneo lake la biashara ili akopeshwe tena nyama,baada ya kukumbushwa deni la nyuma na kukataliwa ombi lake la kukopeshwa tena ndipo akatoa kisu na kumchoma shingoni.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Oska Sanga wameshangazwa na kitendo hicho na kuiomba jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kibedange Rajabu Shayo amesema mtuhumiwa wa tukio hilo anashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako na serikali yake imelazika kumpelekea hosptali aliyechomwa na kisu ili apatiwe matibabu zaidi.