Na Silvia Mchuruza,Bukoba, Kagera
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suruhu Hassan amesema serikali itahakikisha wananchi wanapata huduma Bora ya maji kupitia wizara ya maji.
Hayo ameyazungumza katika hafla uzinduzi wa mradi wa maji wilayani missenyi mkoani Kagera ambapo amesema mradi umegharimu fedha taslimu bilion 15.7 ambao utauduamia zaidi ya watu Laki 7 ambapo itasaidia kuondoa changamoto ya maji.
Ameelekeza wizara ya maji ikopesho milioni Mia 500 kwa mamlaka ya maji Safi na mazingira BUWASA kwa ajili ya kuweza kuwaunganishia wananchi huduma ya maji na kuwataka wananchi kulinda mazingira ya mto Kagera na mradi huo wa maji hili uweze kuwanufaisha.
Pia amewataka wananchi kulipia maji pale watakapounganishwa maji majumbani mwao na watumishi kuacha kuwabambikizia bill nyingi za maji.
Nae Mhandisi mkuu kutoka wizara ya maji Antony sanga amesema kuwa mradi una uwezo wa kuzalisha Lita milioni 8 maitaji Ni Lita milioni 4 na mradi umegharimu bilion 15.7 fedha kutoka serikalini mradi huu utatoa maji ya kutoka na maitaji ya maji yatafikiwa kwa asilimia Mia moja mradi huu umejengwa na kampuni ya CCC ikiwa Ni mradi wa kwanza kutumia CHANZO Cha maji mtoa kagera
“Wizara inawapongeza wajumbe ya bodi ya BUWASA na mwauwasa kwa kuweza kuukagua mpaka mradi huu umefikia kiwango Cha kukamilika na kuondoa changamoto iliyokuwepo “
Juma Aweso waziri wa maji pia ameongeza kwa kusema wizara ya itaendelea kutoa ushirikiano kwa mkoa kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa missenyi na hata mkoa mzima wa Kagera waweze kupata huduma ya maji Safi na salama .
Pia ameongeza kuwa wizara ya maji inakataa kabisa mtumishi wa Aina yoyote kupokea rushwa kwa ajiri ya kufungiwa huduma ya maji na hata wakati wa kusomewa mita serikali aitakubali mtumishi kumdanganya mwananchi katika usomaji wa mita ya maji.
Hata hivyo waziri amewapongeza mainjinia walioshirikiana katika usanifu wa kuanza kujengwa kwa mradi huo katika halmashauri ya wilaya ya misenyi mkoa wa kagera kwa kuhakikisha mradi huo unakubarika katika serikali ya awamu ya 6.