Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) DIT Company Limited.,Dkt.John Msumba,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 9,2022 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaendelea huku akiwaita wananchi kwenda kutembelea Banda la DIT.
WANANCHI Mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika Banda la DIT katika Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaendelea kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
VIONGOZI na Wafanyakazi wa DIT wakiwa katika picha ya pamoja wakati Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaendelea kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAKAZI wa Dodoma na Mikoa ya jirani wameomba kufika katika uwanja wa Jamhuri kujionea kazi nzuri zinazofanywa na Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) DIT Company Limited.
Hayo yameelezwa leo June 9,2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Dkt.John Msumba alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa jamhuri ambapo maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi yanaendelea.
Maonesho hayo yalinza Juni 7 mwaka huu na yanatarajiwa kumalizika June 13 mwaka huu ambapo kesho Makamu wa Rais,Dk.Philip Mpango anatarajiwa kuyafungua.
“Ningependa kuwaomba wananchi waje kwenye banda la DIT waone mambo mazuri yanayoendelea kwani kuna tafiti mbalimbali lakini pia waone huduma mbalimbali tunazozitoa kama Kampuni hii itaonesha sio kufundisha tu bali na kutatua changamoto kwahiyo naawalika wakazi wa Dodoma na Mikoa ya jirani,”amesema Dk.Msumba
Amesema Taasisi nyingi huwa zinabunifu lakini changamoto ambayo huwa inajitokeza ni jinsi gani zinapelekwa kutatua matatizo ya Wananchi.
“Sasa sisi kama DIT tuna hii kampuni tanzu tulianzisha makusudi ili bunifu zote zinazofanywa na wanafunzi ama walimu kuangalia jinsi gani tunazipeleka katika soko,”amesema.
Aidha,Dk.Msumba,amesema ubunifu wa gari kutumia gesi umekuwa ni jambo kubwa kwani kwa sasa wanataka kuipeleka teknolojia hiyo Mikoani.
“Tunafikiria kwenda Mikoani tunashukuru Serikali imeliona hilo na imeongeza vituo vya gesi tunataka yale malengo tuliyojiwekeza tuhakikishe tunayafikia.
“Mmeona bunifu ni nyingi zinatakiwa kuingia sokoni tumepata mwaliko wa Mkuu wa mkoa tutaonesha solution na ataziweka katika Mkoa wa Dodoma,”amesema.