Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameagiza ushiriki wa wilaya na
halmashauri zote za Mkoa Wa Ruvuma kwenye tamasha la Majimaji Selebuka
litakalofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 July 2022 mjini Songea.
Tamasha hili limekua jukwaa kuu la biashara, kutangaza utalii, kuchochea
vipaji, utamaduni , mashindano ya debate kwa shule na michezo, hivyo
linatoa fursa adimu kwa mkoa wetu wa Ruvuma.
Pia mwaka huu
tamasha hili litakuwa na mashindano ya baiskeli ya km 165 toka Songea
hadi Mbamba bay, mbio na mpira wa miguu na kikapu. Ili kuwapa urahisi
washiriki kwenye Majimaji Selebuka imezindua tovuti yenye zaidi ya
hoteli 200 kwa ajili wageni.
Pamoja na kutangaza vivutio vya
utalii vya mkoa wa Ruvuma, Majimaji Selebuka inachochea biashara, elimu,
sanaa, michezo kwenye ukanda wa kusini
Majimaji Selebuka ni
tukio linalofanyika kila mwaka Songea, Ruvuma ambapo mwaka huu
litazizima kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai. Kujisajili ingia
majimajiselebuka.co.tz