Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania PLC, George Lugata (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya kisasa aina ya Samsung Galaxy A73 5G ambayo itapatikana kwenye maduka yote ya Vodacom nchi nzima ikiwa na ofa ya intaneti ya 8GB kila mwezi bure kwa mwaka mmoja. Kushoto ni Meneja mkazi Samsung Tanzania, Manish Jagra na Mkuu wa Mauzo na Masoko Samsung Tanzania, Moses Mtweve. Ujio wa simu hii utaongeza matumizi ya vifaa vya kidijitali nchini.
**************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR S SALAAM
KATIKA kuhakikisha wateja wao wanakuwa na data nzuri na yenye ubora zaidi, Kampuni ya Vodacom Tanzania imeingia makubaliano ya kuitangaza simu mpya aina ya Samsung Galaxy A73 5G yenye ubora wa hali ya juu.
Akiungumza wakati akiitangaza simu hiyo , Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw.George Luyata amesema Vodacom wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha wanakuwa na data nzuri ambapo kwasasa wanaongoza katika mitandao yote nchini kwa kuwa na speed ya 4G ambayo imekuwa bora zaidi.
“Tanzania tume Cover asilimia 92 katika mikoa yote minara yetu yote ina 4G kwahiyo tuko vizuri na tunaubora unaotakiwa”. Amesema
Amesema mteja atakaenunua simu hiyo ya Samsung Galaxy A73 5G atajipatia 8GB kila mwezi kwa miezi 12 hivyo amewashauri wateja wa Vodacom kutembelea maduka yao yaliyopo karibu ili waweze kujipatia simu hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mauza na Masoko wa Kampuni ya Samsung Tanzania Bw.Moses Mtweve amesema ili kuendelea kuboresha biashara yao kwa wateja wao ni lazima wajiunge na kampuni ambayo ya mtandao unaofanya vizuri ili waweze kuendana nao katika kumfikishia mteja huduma iliyobora zaidi.
amesema Samsung Galaxy A73 5G imekuwa simu ambayo imeboreshwa kuanzia kwenye betri pamoja na kamera ili kuhakikisha mteja wao anafurahia huduma kutoka kampuni hiyo.
“Kama simu yako imekreki tunaweza tukaibadilisha screen yako kwa bure kabisa yaani utachangia kiasi kidogo cha matengenezo ambacho ni asilimia ndogo sana kwahiyo hii ndo kati ya ofaa ambayo tunatoa lakini tumejiunga na wenzetu Vodacom ambao nao wameweka ofa yao ya bando ambalo utalitumia kwa mwaka mzima”. Amesema