Waziri wa Katiba na Sheria Dr.Damas Ndumbaro amemuagiza Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara kuhakikisha Mahakama iliyojengwa na Serikali katika eneo la Haydom kuanza kazi June 30 mwaka huu ili kuokoa gharama kwa Wananchi wanaosafiri umbali mrefu kwenda Mbulu kusikiliza mashauri yao.
Dr. Ndumbaro amesema hayo akiwa Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wakati akikagua Ujenzi wa Mahakama ya mwanzo ya Haydom ambayo Serikali kupitia kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 450 kukamilisha ujenzi wa Mahakama hiyo ambapo Wananchi walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Km 86 kufuata huduma ya Mahakama.
“Kutoka hapa mpaka Mbulu nauli ni shilingi elfu sita,kwenda na kurudi ni shilingi elfu kumi na mbili na utaratibu wa Mahakama unakwenda angalau mara moja kila mwezi,kwa miezi 12 jumla unatumia nauli shilingi laki moja na elfu arobaini na nne(144,000) ukilala utalipa 10,000 kwenye chakula na elfu kumi nyingine kwenye malazi jumla ni 20,000 gharama hii kwa miezi 12 ni laki mbili na arobaini (240,000) ambapo jumla kuu inakuwa Sh.384,000 hizo ndiozo gharama ambazo mlikuwa mnazitumia tena kwa kiwango cha chini kabisa, leo Serikali imeleta milioni shilingi milioni 458 mahakama ile itakabidhiwa rasmi tarehe 13 mwezi huu” Dr Ndumbaro
Nao wananchi wa Wilaya ya Mbulu wamesema baadhi wananchi ambao walikuwa wakishindwa kumuda gharama za nauli kwenda kusikiliza mashauri yao wakati mwingine walikuwa wakipoteza haki zao,hivyo uwepo wa Mahakama hiyo kutasaidia upatikanaji wa haki kwa kila mwananchi