Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwa na baadhi ya kinamamma, wakionesha tuzo maalumu iliyotolewa kwa Rais Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na wanawake wa Mkoa wa Mtwara kwa kutambua na kumpongeza kutokana na kazi nzuri anayoifanya katika kuongoza nchini. (Picha na Fahad Siraji wa CCM).
Wananchi wa Eneo la kiwanja Cha NDEGE Wakiwa wamenyanyua mabango yenye jumbe mbalimbali katika kupata utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa eneo la kiwanja cha ndege mkoani Mtwara na mamlaka ya viwanja vya ndege.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka,Akizungumza alipotembelea eneo lenye mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa eneo la kiwanja cha ndege mkoani Mtwara na mamlaka ya viwanja vya ndege.alipofuatilia maelekezo aliyoyatoa alipotembelea eneo hilo la mwaka 2021, Shaka amesema danadana hizo hazina tija kwa wananchi na kutoa maelekezo kwa wizara nne kukutana haraka ili kuutafutia ufumbuzi mgogoro.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akikagua baadhi ya maeneo yanakopitia makaa ya mawe zikiwa ni hatua za kuyapokea, kuyahifadhi na kuyasafirisha kwenda nchi mbalimbali.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akikagua Sheena ya pembejeo za kilimo kwa ajili ya wakulima wa korosho mkoani Mtwara.
**************************
Wanawake mkoani Mtwara, wamemkabidhi tuzo maalumu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wa kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo hususan mkoani humo.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema tuzo hiyo itamtia moyo na kumpa ari Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania.
“Kitendo cha kumpatia tuzo mnamtia moyo, mnapa ari ya kuwatumikia Watanzania, lakini pia mnamtia ari ya kutimiza malengo yenu akinamama katika mambo muhimu na ya msingi kama ambavyo nimeshasema.
“Wito wangu kwenu msisite, msiishie hapa endeleeni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu, kila mmoja kwa imani yake Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema ili aweze kututumikia Watanzania,” amesema.
Akiendelea kuzungumza zaidi kuhusu tuzo hiyo, Shaka amesema aliyoyafanya Rais Samia wanawake wanayajua hata ukiwaamsha usingizini wanakwambia ameifungua Mtwara.
Awali akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, kwa niaba ya wanawake hao Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mtwara, Zuhura Farid, amesema wanawake wa Mtwara kwa niaba ya wanawake wengine wote wanampongeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya.
“Hivyo tunaomba tukukabidhi zawadi hii kwa heshima na taadhima tunaomba umfikishie zawadi hii mama na umwambie asichelewe kufika Mtwara aje atuone kinamamma,” amesema.