NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini leo ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa huo Bw. Abdallah Mohamed Malela. Aliyeambatan
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na baadhi ya askari na maafisa wa Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Idara ya Uhamiaji pamoja na wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wa Mkoa wa Mtwara leo, Juni 4, 2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani humo.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa huo Rehema Madenge, tarehe 3 Juni 2022 ikiwa moja ya ziara yake katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,tarehe 3 Juni 2022 ikiwa moja ya ziara yake mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt Anna Makakala baada ya kutembelea Ofisi ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam,
…………………………………………….
Na Mwandishi wetu,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewataka Askari na Maafisa waliopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutumia fursa walizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuongeza nguvu zaidi katika utendaji kazi hali itakayoendelea kuleta tija katika kuleta amani na utulivu wa Nchi.
Akizungumza na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Usalama vya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi vilivyomo mkoani Lindi na Mtwara katika nyakati tofauti, Naibu Waziri Sagini amesema kuwa ndani ya Mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu ,Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha ajira mpya, ameongeza mishahara na ameruhusu upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa waliopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
“Kwa kutambua mchango wenu mkubwa wa kuleta amani na utulivu katika nchi yetu Rais Samia Suluhu Hassan ametuthamini sana katika kazi zetu kwa kutupatia ajira mpya, kupandishwa vyeo na ongezeko la mishahara, sasa matarajio yetu ni kwamba mtaongeza nguvu katika utendaji kazi wenu kwa kufuata Maadili na Sheria za Nchi” alisema
Aidha Naibu Waziiri Sagini amesema Rais Samia amefanya mageuzi makubwa ya kibajeti kwa ajili ya kuwezesha Vyombo vya Usalama nchini vya Wizara ya Mambi ya Ndani ya Nchi vipate nyenzo ya kuendeleza na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kikazi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara yenye lengo la kukagua Miradi ya ujenzi wa Idara ya Uhamiaji yaliyopo Mkoani Lindi na Mtwara, kujitambulisha na kuongea na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mikoa hiyo.
Pia aliwataka Viongozi wa Vyombo vya Usalama wa mikoa hiyo kuendelea kusimamia maadili ya askari waliopo chini yao na kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata Sheria za nchi.
“Matarajio yetu kama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kuona nidhamu na utii wa Sheria kwa askari na maafisa. Kama kiongozi wetu, Rais Samia amefanya mambo mema namna hii sisi tunamlipa nini? ni matarajio yake kuona utumishi uliotukuka.”
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala amewataka Maafisa na askari hao kuendelea kufanya kazi kwa utii, uhodari na weledi wa hali ya juu. Aidha amehimiza upendo mshikamano, uwajibikaji na kukataa rushwa.