AFISA Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dalia Charles,akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
Mkutubi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Cecilia Doualas,akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
AFISA Elimu ya Jamii kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Suzan Chawe,akimsikiliza mwananchi alipotembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
AFISA Mazingira Mwandamizi Kanda ya Kati kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kawa Kafuru,akiwapa elimu wananchi waliotembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
AFISA Mazingira Mwandamizi Kanda ya Kati kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kawa Kafuru,akizungumza na waandishi wa habari kwenye Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
AFISA Elimu ya Jamii kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Suzan Chawe,akielezea jinsi walivyoweza kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembeleaBanda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
…………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
NEMC yatoa neno kwa wananchi,wafanyabiashara na wawekezaji katika maonesho ya mazingira Dodoma
WADAU mbalimbali wameendelea kujitokeza katika Banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambao maonesho ya wiki ya mazingira yanaendelea.
Baraza hilo limewasihi wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji waendelee kutii Sheria na Kanuni zinazosimamiwa na Baraza hilo.
Wananchi wakiwa katika banda hilo wamekuwa wakipatiwa elimu pamoja na kuelezwa shughuli mbalimbali ambazo zinafanywa na NEMC.
Wadau ambao wamejitokeza ni pamoja na wafanyabiashara, wanafunzi, wakulima, wawekezaji na wananchi kwa ujumla ambao wengi wamefurahia huduma ambazo zinatolewa na Baraza hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la NEMC Afisa Mazingira wa NEMC Kanda ya Kati, Kawa Kafuru amesema wameshiriki katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili waweza kujua mambo mbalimbali yanayofanywa na Baraza hilo.
“Tunafanya uelimishaji kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ulimaji bora wa mazao kwa mazao yanayohimili ukame, tunaelimisha wale wenye miradi ya mazingira waone umuhimu wa kusajili ikiwa ni pamoja na kufanyiwa ukaguzi.
“Tunasimamia uwepo wa mifuko ambayo haina ubora ili kuhakikisha mifuko ambayo haina ubora inaondolewa, tunaendelea kuwasihi wananchi kutumia mifuko ambayo imethibitishwa na Serikali.
“Tunatoa elimu wawekezaji kulipa toza za kimazingira kwani tunaelekea mwisho wa mwaka. Niendelee kuwasihi wananchi na wafanyabiashara na wawekezaji waendelee kutii Sheria na Kanuni zinazosimamiwa na Baraza.
Afisa Elimu Jamii NEMC, Suzan Chawe amesema sehemu kubwa ya maonesho yanazingatia zaidi elimu kwa jamii juu ya shughuli wanazofanya pamoja na huduma ambazo watu mbalimbali wanaweza kuzipata.
“Tumepokea wageni wengi katika banda letu wengi wamekuwa na shauku ya kujua mchakato wa mazingira unaendaje hasa wa kupata cheti pamoja na gharama pia wanafunzi wengi wamepata namna ya kuwa washauri elekezi sisi tunawasajili na ni sehemu ya ajira na tumewaelekeza namna ya kufanya wengi bado wapo mashuleni,”amesema.