Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor akisalimiana na watumishi mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipotembelea ubalozi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akisaini kitabu katika Ofisi ya Balozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipotembelea Ubalozi huo leo tarehe 4 Juni 2022 (kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mheshimiwa Grace Olotu).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akitazama picha za kumbukumbu ya Mabalozi waliowahi kuhudumu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipotembelea Ubalozi huo leo tarehe 4 Juni 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akikagua ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipotembelea Ubalozi huo leo tarehe 4 Juni 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Balozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipotembelea Ubalozi huo leo tarehe 4 Juni 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Grace Olotu, Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Simbachawene, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Dkt. Omary Shajak na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden wakati alipofika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden leo tarehe 4 Juni 2022 Mjini Stockholm.
…………………………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amewaasa watumishi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kuongeza maeneo ya ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hiyo ili kuchangia vema katika diplomasia ya uchumi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 4 Juni 2022 alipotembelkea Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden uliopo Mjini Stockholm. Amesema ni vema kudumuisha mahusiano mazuri yaliopo baina ya mataifa hayo mawili ambao umedumu kwa muda mrefu.
Makamu wa Rais ameongeza kwamba nchi ya Sweden imekua rafiki kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali kama vile katika sekta ya Elimu, Utawala bora pamoja na Uchumi. Aidha amewasihi kutafuta zaidi ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji pamoja na fursa za za masomo zitakazosaidia katika kuwajengea uwezo watanzania wa kufanya kazi.
Aidha Makamu wa Rais ameuagiza Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kuhakikisha wanajenga mtangamano kwa watanzania wanaoishi Sweden pamoja na maeneo mengine ya uwakilishi ili waweze kuwa na mchango katika ujenzi wa Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mheshimiwa Grace Olotu amesema Ubalozi huo utaendelea kuwatumikia watanzania katika maeneo yote ya uwakilishi kwa kuitangaza na kuhakikisha wanaendeleza diplomasia ya uchumi kwa tija kubwa kwa manufaa ya taifa.