MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ,akiongoza zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akimuangalia Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji Masoko na Teknolojia REA Mhandisi Edvera Mwijage ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA,akipanda Mti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala,akipanda mti Mti katika Hospitali hiyo kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
Balozi wa Mazingira Aneth Andrew ambaye pia ni Mwandishi wa Habari TBC akipanda mti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
WATUMISHI wa REA wakipanda miti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji Masoko na Teknolojia REA Mhandisi Edvera Mwijage ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA,(kushoto) akizungumza mara baada ya kupanda Miti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro, akiipongeza REA kwa kuendelea kuiweka katika mazingira bora Dodoma ya kijani mara baada ya REA kupanda Miti katika Hospitali ya Mirembe zoezi lililofanyika leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
Afisa Mazingira REA, Aziz Abbu ,akielezea walivyoshiriki katika maadhimisho ya siku ya mazingira kwa kuchangia zoezi la upandaji miti katika hospitali ya Mirembe.
KATIBU Mtendaji Habari Development Association Bernard Mwanawile,akizungumza jinsi walivyojipanga kuitunza na kuilinda Miti hiyo.
WATUMISHI wa REA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda miti katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo kwa ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma.
……………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ameipongeza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa kupanda miti zaidi ya miti 2000 katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe kwa lengo la kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wa akili wanaokuwepo katika Hopitali hiyo.
Akizungumza leo Juni 4,2022,Jijini Dodoma wakati wa zoezi la upandaji wa miti hiyo,Shekimweri amesema wanaamini katika mazingira ndio maana REA wameamua kupanda miti hiyo katika Hospitali ya Mirembe.
“Niwapongeze REA kwa kuunga mkono program ya kupanda miti nimefarijika sana.Nyinyi sio mmeshiriki tu pia mmetoa ufadhili niwahakikishie nitafuatilia na mnapofuatilia ningependa niwepo.
“Naomba Jumanne(wiki ijayo) mje na huo mkakati ili tuone hapa mnafanya nini mnaposema Programu ya utalii itaakisi kwenye nini?Hichi ni kitu kikubwa tusikifanye kwenye udogo nimefarijika sana tunawaunga mkono na miti hapa itatunzwa vizuri sisi tutaendelea kuwaunga mkono,”amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji Masoko na Teknolojia REA Mhandisi Edvera Mwijage ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA, amesema wanaamini katika mazingira ndio maana wameamua kupanda miti hiyo katika Hospitali ya Mirembe.
“Kama Taasisi tulipoapata hili ombi tuliona ni lazima tushiriki kutunza vyanzo vya maji sisi kama Rea tunaamini tukitunza mazingira vizuri maji yatapatikana na mvua tutapata za kutosha.
“Taasisi tunaamini katika mazingira kuna utulivu wa akili, ukuaji wa hii miti unatoa fursa kwa wagonjwa wetu kukaa na kupata amani ya akili.
“Mikakati tuliyonayo hapa ni karibu kama ofisi tutakuwa tunatembelea mara kwa mara kuangalia kama inamwagiliwa kwani kupanda ni kazi moja ila kukua ni suala lingine na hii miti itamwagiliwa na kukuwa kwa idadi kama ilivyopandwa,”amesema.
Naye,Afisa Mazingira REA, Aziz Abbu amesema wameamua kushiriki katika maadhimisho ya siku ya mazingira kwa kuchangia zoezi la upandaji miti katika hospitali ya Mirembe.
“Tunashiriki kwa vitendo katika suala la utunzaji wa mazingira kwa kupeleka nishati bora tunashiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kupeleka huduma hiyo kwa wananchi.Tumeamua kushiriki eneo hili ni karibu na Hospitali ya Mirembe tunatarajia kuendelea kushiriki katika mazoezi ya namna hii,”amesema.
Awali Mkuu wa Idara ya mazingira jiji la Dodoma Dickson kimaro, amesema Dodoma ya kijani inawezekana kwani miti inayopandwa zaidi ya asilimia 80 ni lazima iote.
“Kwa Mirembe katika miti 200 ambayo tumepanda nimeona yote imeota maana yake hata kipindi cha kiangazi wanauwezo wa kupanda miti kikubwa ni itunzwe na shimo liwekwe mbolea,ardhi ya Dodoma ina shukrani kwani miti inakuwa,”amesema.
Hata hivyo,Kimaro ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kupanda miti ya vivuli pamoja na matunda kwani watakuwa wametunza mazingira.