Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzani (CCWT) Jeremieh Wambuara akizungumza na Wafugaji Wilayanj Chunya kuhusiana wafugaji kushiriki Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022.
Wafugaji wakisikiliza mada kuhusiana Sensa ya Watu na Makazi 2022.
*************
*Wafugaji kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi kusaidia kupanga mipango.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Jeremiah Wambura anaendelea na ziara yake katika mikoa yote Tanzania Bara ambapo Junii 2, 2022 alizuru katika Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungunza na wafugaji Wilaya ya Chunya.
Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi mbalimbali Jijini Dar es salaam jana Wambura, alisema lengo kubwa ni kuhakikisha wafugaji wanashiriki vyema kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi, kujiandaa kuhesabiwa pamoja na zoezi la utambuzi wa Mifugo lakini pia kufanya usajili wa mifugo ya wafugaji.
“Ninazisisitiza Halmashauri zote ambazo hazijafanya hivyo kuanza mara moja kwani ukomo wa usajili wa mifugo kwa hihali ni Agosti 31, mwaka huu lakini pia sensa ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa,”alisema Mwenyekiti Wambura.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa ameamua kufanya ziara hiyo ili kuwahamasisha wafugaji kushiriki vyema lakini pia kuwakumbusha kuwa ki hitimisho lake ni 23/08/2022.
“Nikiwa mwenyekiti wa wafugaji Tanzania ni wajibu wangu kuwakumbusha wafugaji mambo muhimu wanayotakiwa kuyafanya kwa ajili ya maendeleo yao na mifugo yao,” alisema Mwenyekiti Wambura na kuongeza ;
“Sio wote wenye uelewa kuhusiana na mambo haya na ndio maana nimeamua kufanya ziara kwa ajili ya kutoa elimu ili waweze kuelewa na kuwa tayari kwa ajili ya kutoa ushirikiano,”alisema Mwenyekiti Wambura.
Mwenyekiti kwenye ziara yake aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ukaguzi na Haki za Wanyama kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Annete Kitambi, Mratibu wa Sekta ya Mifugo kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI Dkt. Bertha Dugange.
Aidha Dkt. Annete alieleza sifa za utambuzi na kusisitiza wafugaji kuekeza kwenye ujenzi wa miundombinu na upandaji wa malisho.
Naye Mratibu wa Sekta ya Mifugo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Bertha Dugange alisistiza juu ya ushirikiano wa Wadau katika mnyororo wa thamani wa Sekta ya Mifugo na kuhamasisha wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.