Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Dkt. Respisious Boniface akisaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Kampuni ya Smart Tech Solution kuongeza kiwango cha mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa. Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Dkt. Respisious Boniface Madaktari bingwa wa mifupa kutoka katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wakiwa katika mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa yaliyofanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo Juni 3, 2022 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa yaliyofanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo Juni 3, 2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Dkt. Respisious Boniface akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa yaliyofanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo Juni 3, 2022 Jijini Dar es Salaam
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa yaliyofanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) leo Juni 3, 2022 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Kampuni ya Smart Tech Solution kuongeza kiwango cha mafunzo ya Matibabu ya vyuma kwa wagonjwa waliovujika mifupa.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo ya siku mbili katika hospitali hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Dkt. Respisious Boniface amesema matibabu hayo yanatajwa kupunguza muda wa mgonjwa kupona kutoka miezi mitatu na minne hadi mwezi mmoja.
“Upasuaji wa kisasa ni kuweka vyuma ambapo mgonjwa anachukua muda mfupi kupona mfano mfupa mrefu wa paja tukiweka vyuma mgonjwa anakaa siku tatu ya nne anaondoka ,anakuja kliniki na baada ya mwezi ameshapona”. Amesema Dkt. Boniface.
Aidha amesema kabla ya njia ya kisasa walikuwa wanafunga mawe hivyo mgonjwa huchukua miezi miwili mpaka mitatu kupona kwa teknolojia ya vyuma anapona muda mfupi.
Amesema nia ya mafunzo hayo ni kuboresha huduma za tiba kama ilivyo nia ya Rais Samia na mafunzo hayo yanahusisha madaktari wa ngazi ya Mikoa,Wilaya na Kanda ambapo kwa kiasi kikubwa wameweza kushiriki.
Pamoja na hayo Dkt.Boniface amesema Kampuni ya Smart Tech Solution inawatafutia mafunzo huko nchini Misri na watakuja kutoa mafunzo hapa na kwa nje wao watadhamini mafunzo.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Mifupa Dkt.Rabinde Serua amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuendeleza maendeleo ya kujenga uwezo wa madaktari jinsi ya kutibu mifupa ndani na nje ya taasisi.
“Kuna waliotoka hospitali za Wilaya,Mikoa na kanda na pia tumepata vifaa mbalimbali kwaajili ya mafunzo na kwaajili ya kutibu wagonjwa wetu,”ameeleza.
Amesema kuwa kabla ya mafunzo haya wagonjwa wengi walikuwa wanatoka sehemu mbalimbali wanachukua muda kufika MOI hivyo sasa matibabu yatafanyika katika hospitali za wilaya na mikoa.