Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisaini kitabu cha wageni cha Ofisi ya CCM Kata ya Imalaseko wilayani Meatu, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Mzee Lucas Maganga. Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya Kuangalia uhai wa Chama pamoja Kukagua na Kuhamasisha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 katika mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Imalaseko wilayani Meatu. Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya Kuangalia uhai wa Chama pamoja Kukagua na Kuhamasisha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 katika mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Meatu Leah J. Komanya (kulia) wakati wa mkutano na wanachama wa kata ya Ng’hoboko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiwahutubia wanachama wa CCM kata ya Ng’hoboko wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wilayani Meatu mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Vijana wa Sungusungu kwenda kwenye eneo la mradi wa maji Isengwa, Meatu mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Isengwa, wengine pichani kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed na kushoto ni Mkuu wa Mkoa Ndugu David Kafulila.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Isengwa kutoka kwa Meneja wa RUWASA Meatu Mhandisi George Massawe.
Mbunge wa Jimbo la Meatu NMhe. Leah J. Komanya akiwa amempakata mtoto wa mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa Shina Mwandu Itenje ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.