Mkurugenzi wa Cecy Toto & Gift Shop Cecilia Melchior akizungumza na wanahabari kuuhusu wazazi kuwakinga watoto wao dhidi ya baridi
Cecilia Melchior Mkurugenzi wa Kampuni ya Cecy Toto & Gift Shop
…………………………………………………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wazazi wameshauriwa kuwakinga watoto wao dhidi ya baridi ili kuweza kuwanusuru na magonjwa mbalimbali ikiwemo pumu.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Cecy Toto&Gift Shop Cecilia Melchior wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya malezi na makuzi kwa watoto.
Amesema katika kipindi cha baridi kunahatari kubwa sana ya watoto kuugua ugonjwa wa nimonia,pumu hivyo ni vyema wazazi wawe makini kuwastiri kwa kuwavalisha mavazi mazito.
Melchior ameeleza kuwa aliamua kujihusisha na uuzaji wa vifaa vya watoto baada ya kuwa amejifungua akiwa katika mazingira ya kufanya kazi za kuajiriwa ambapo hakupata muda mzuri wa kumle mtoto.
” Mtoto anahitaji malezi mazuri na yakaribu ili aweze kukua katika afya njema, nilivyojifungua nilibanwa sana na kazi hali iliyonifanya nikashindwa kumuhudumia Mwanangu ndipo nilipo amua kuacha kazi na kifungua duka la vifaa vya watoto na wanawake wajawazito”,amesema Melchior
Amesema pamoja na huduma anayoitoa ya kuuza vifaa vya watoto na wanawake wajawazito,pia ameendelea kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa watoto sanjari na kuwapatia elimu wamama wajawazito ikiwemo ya kupaka mafuta kwenye tumbo ili kuweza kuepukana na michirizi ambayo husababisha tumbo kupoteza uhalisia wake.