Mkuu wa tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Suma JKT leo Mei 31,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana waliohitimu elimu ya Sekondari kidati cha Sita kwa mwaka 2022 waliopangiwa makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo kuripoti makambini kuanzia Juni 3 hadi 17,2022.
Akizungumza wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Mei 31,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema orodha kamili ya majina walioitwa, makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo yaliyopo pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz
Aidha amesema kuwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.