Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipokea kombe la Dunia kutoka kwa Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti katika hafla ya kupokea kombe hilo leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi mfano wa kombe la Dunia kutoka kwa Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti katika hafla ya kupokea kombe hilo leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti katika hafla ya kupokea kombe hilo leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti katika hafla ya kupokea kombe hilo leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti katika hafla ya kupokea kombe hilo leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Brazili Juliano Belletti akizungumza katika hafla ya Tanzania kupokea kombe la Dunia, hafla iliyofanyika leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kupokea kombe la Dunia leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt.Hassan Abbas akizungumza katika hafla ya kupokea kombe la Dunia leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Baadhi ya wachezaji wa zamani wa Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu nchini wakifuatilia hafla ya kupokea kombe la Dunia, leo Mei 30,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
( PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
Na John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amepokea kombe la Dunia la FIFA Ikulu jijini Dar es Salaam ambalo litakaa kwa siku mbili kabla ya kuondoka kesho kutwa.
Kombe hilo amekabidhiwa na mchezaji mkongwe duniani wa Brazil Juliano Belletti ambaye anaongoza timu ya ziara ya kombe hilo nchini.
Akipokea kombe hilo Rais Samia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Juni 1, 2022 kufika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kupiga picha na kombe hilo.
Tanzania inakua miongoni mwa nchi tisa za Afrika ambazo imepata bahati ya kupitiwa na kombe hilo.
Mhe. Samia amefafanua kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa miongoni mwa nchi hizo kutokana na kuendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ambapo amesema watanzania wengi wanapenda soka.
Kesho kombe litaanza kuonyeshwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni na baada ya hapo kutaonyeshwa filamu ya Royal tour ambayo Mhe. Rais Samia ameshiriki.
Mhe. Rais ametoa rai kwa watanzania kutumia ujio wa kombe la Dunia nchini kuitangaza Tanzania duniani.
Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, amemshukuru Mhe.Rais kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye Michezo katika kipindi kifupi cha utawala wake.