Afisa
Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga
Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wananchi walofika kwenye Banda lao
lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya biashara
kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda
Afisa
Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga
Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi
walofika kwenye Banda lao
lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya
biashara kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda
Maafisa
wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga
wakiwahudumia wananchi kama wasikiliza kwa umakini wananchi
waliotembelea banda lao katika ni Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Tanga Hadija
Mpungu kulia ni Afisa Mwandamizi wa NSSF Muheza Fatma Ally kushoto ni
Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda
Afisa
Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga
Abubakari Mshangama katika akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa
Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Tanga (TCCIA) Rashid
Mwanyoka kushoto wakati walipotembelea banda lao
Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari. |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MFUKO
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) Mkoani Tanga umesema kwamba
wanatumia maonyesho ya Biashara ya mwaka 2022 yanayoendelea kwenye
viwanja vya mwahako kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa mbalimbali
zinazopatikana kwenye mfuko huo
Hayo yalisemwa
leo na Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga
Abubakari Mshangama wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho
ya Biashara.
Alisema kwamba uwepo wa maonyesho hayo ambayo
hufanyika kila mwaka umekuwa na tija na kwa na bahati nzuri mwaka huu wao
wamekuwa moja ya wadhamini hivyo wameona fursa nyingi zinatokea pamoja na kuwa
na mkutano na wafanyabiashara na wao kuelezea changamoto walizokuwa
nazo na nini kuboreshwe na nini kiongezwe kwenye huduma wanazotoa kwa
mkoa huo.
“Kwa kweli niwaambie kwamba maonyesho ya mwaka huu
yamefana kuliko yalivyokuwa miaka iliyopita kutokana na washiriki
wamekuwa wengi kutoka 62 mpaka 95 mwaka huu na hiyo ni faida kwetu kwani
tumeweza kuandikisha wanachama 53 na waajiri wapya wawili”Alisema
Aliongeza
kwamba hatua hiyo inawaweka vizuri katika malengo yao na inawasaidia
kuongeza wanachama na kuongeza michango inayofikia kwenye malengo yao ya
wanachama wa Sekta ya viwanda na Utalii ambapo kuna wajasiriamali
wadogo kupitia NSSF sekta isiyokuwa rasmi wanaweza kuongea nao na
kuweza kuwapa elimu na wawo kuweza kuwapa mapendekezo ya aina gani ya
mafao watakayopenda .
Hata hivyo alisema tokea kuanza mwa
maonyesho hayo mpaka sasa wamekwisha kuandikisha wanachama 51 na waajiri
3 huku lengo lao la siku 10 za maonyesho hayo waandikishe wanachama
wapya 230 na waajiri 14.