Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Athony Mavunde (katikati) akikata utepe rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na Kilimo chini ya Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth unaofadhili wa USAID kutoka nchini Marekani.
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Athony Mavunde akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na kilimo chini ya Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth unaofadhili wa USAID kutoka nchini Marekani
Mkurugenzi wa Misheni USAID Bi. Kate Somvongsiri ambao ni wafadhili wa Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na Kilimo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth Bi. Ngasuma Kanyeka akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na kilimo chini ya Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth unaofadhiliwa na USAID kutoka nchini Marekani.
Wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na kilimo chini ya Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth unaofadhili wa USAID kutoka nchini Marekani uliofanyika leo jijini Dar es Salaaam (Picha na Noel Rukanuga)
*********************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth imezamilia kuendelea kuwasaidia vijana kwa kuweka mazingira rafiki katika sekta ya kilimo ikiwemo upatikanaji wa ardhi, pembejeo, masoko pamoja na mitaji jambo ambalo litawasaidia vijana kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha mafanikio ya vijana wanaojishughulisha na Kilimo chini ya Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth, Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Athony Mavunde, amesema kuwa vijana wengi wanapenda kushiriki katika sekta ya kilimo ila changamoto ni upatikanaji wa ardhi ya kilimo pamoja na pembejeo.
Mhe. Mavunde amesema kuwa serikali imejipanga kuwatafutia vijana ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo na masoko ya mazao yao, kuweka miundombinu rafiki, kuwapatia pembejeo pamoja na kuanzisha kijiji cha kilimo cha vijana, ambapo watakuwa wanafanya kazi ya kilimo katika eneo hilo.
“Nchi yoyote inayopenda kuendelea kwa haraka lazima katika uzalishaji vijana washiriki, wizara ya kilimo imejiwekea malengo ili kuiona sekta ya kilimo inakuwa kwa asilimia 10 hadi kufikia mwaka 2030, lakini hivi sasa inakuwa kwa asilimia nane, sisi tumekwenda mbali zaidi” amesema Mhe. Mavunde.
Amesema kuwa moja ya kitu muhimu ni kuongeza nguvu kwa vijana kwa kuweka mipango ambayo ni rafiki katika kufikia malengo tarajiwa.
Mhe. Mavunde amebainisha kuwa kuanzia mwezi July mwaka huu serikali itaaza rasmi mpango wa kuanzisha kijiji cha kilimo cha vijana katika Wilaya ya Bahi na Chamwino Mkoani Dodoma, ambapo vijana watapata fursa ya kuwekewa miundombinu rafiki na kuanza kulima zao la alizeti.
“Tumetenga ekari 20,000 katika Wilaya ya Bahi na Chamwino kwa ajili ya kilimo kwa vijana na tutaaza na Mkoa wa Dodoma na baadaye nchi nzima hasa katika maeneo ambayo viongozi watakuwa tayari kutoa eneo, kama kutakuwa na ugumu tupo tayari kufidia ili kufikia malengo tarajiwa” amesema Mhe. Mvunde.
Mhe. Mavunde ameipongeza USAID kwa kufadhili mradi Feed the Future Tanzania Advancing Youth na kufikia malengo tarajiwa pamoja na wizara yake kupewa magari mawili kwa ajili kwenda kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya vijana katika sekta ya kilimo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth Bi. Ngasuma Kanyeka, amewapongeza vijana kwa kuonesha jitiada na kufanikiwa kufikia malengo na kustahili kupata uwekezaji huo.
Hata hivyo ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika fanikisha mradi huo ambao umezaa matunda kwa vijana na kufanikiwa kupiga hatua kiuchumi.
Rais wa Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Paul Koyi, amesema kuwa wapo tayari kuwajibika kusaidiana na wizara ya kilimo katika kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu na sekta ya kilimo na kusonga mbele.
Amesema kuwa mradi huo ambao umefikia mwisho na ameona vijana wamepiga hatua kubwa ya kimafanikio na kufikia malengo yao tofauti na awali.
“Tupo kwa ajili ya kuwasaidia vijana waweze kupiga hatua zaidi katika mafanikio na tunawakaribisha kujiunga na Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) ili walipe kodi kupitia biashara zao” amesema Bw. Koyi.
Hata hivyo vijana hao watano walionufaika na mradi wa Feed the Future Tanzania Advancing Youth na kubadilisha maisha yao kichumi, wameonekana kuwa na furaha huku wakiishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kutoa.