Meneja wa kituo cha Sayansi Maxi George akizungumza wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kilipoanzishwa
Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali
Na Oscar Assenga,TANGA
Kituo cha Sayansi cha Stemp Park
kilichopo Jijini Tanga kimeleta Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya elimu
ambapo kimeweza kuwa kichocheo kwa Wanafunzi kuhamasika kupenda kusoma
Masomo ya Sayansi na kuongeza ubunifu.
Stemp Park ipo katika kata ya Kisosora na imeleta mapinduzi makubwa katika masomo ya Sayansi kwa Wanafunzi pamoja na Walimu.
Wanafunzi wanaotumia kituo hicho katika mambo ya Sayansi ni kianzia Chekechea hadi shule za Sekondari.
Akizungumza
juzi katika wiki ya Sayansi Afrika Meneja wa kituo hicho Maxi George
wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa
Kwake iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya sayansi katika bara
la Afrika
Ambapo alisema idadi kubwa ya ubunifu wa kisayansi
katika jiji la Tanga umekuwa mkubwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakienda
kituo hicho na kufanya shughuli zao za ubunifu ambapo wanafanya wa
nadharia zaidi.
“Hapa vijana wanapata nafasi ya kuelezwa umuhimu
wa Sayansi katika maisha ya kawaida,na katika maisha ya shule kwa
kujifinza mambo mbalimbali ya sayansi kwa vitendo na kwa kuona”alisema
George
Katika hatua nyingine kituo hicho pia kinawanufaisha
walimu wa mkoa wa Tanga kwa kuwapa ujuzi katika kuwafundisha wanafunzi
shuleni
“Walimu wanaprogram maalum ambayo inaitwa TOT hii imekuwa
chachu ya kuwapa ujuzi katika kuwafundisha vijana,lengo likiwa ni
kuchagiza ufaulu kwa masomo ya sayansi”alisema George
Pia
aliwaasa wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wajifunze masomo ya
Sayansi kuwa sio ngumu bali watu waliaminiashwa kuwa ni ngumu
“Tunatoa
wito kwa Wazazi,kuwaachia watoto wajifunze zaidi,pale mtoto anapofanya
jambo la ubunifu mzazi amwache akifanye ili apate njia sahihi ya
kutengeneza kitu anachokitaka ambacho badae kinaweza kuwa na
manufaa”alisema George
Aidha Wanafunzi wanaoenda kwenda kujifunza katika kituo hicho wameeleza kuwa kituo hicho kimewajenga zaidi kwa kuwa wabinifu.
Mmoja
wa wanafunzi wa kike Rukia Omari wa Masechu Sekondari anayenda kupata
elimu ya Sayansi katika kituo hicho alisema wao wanakabiliwa na
changamoto pindi wanapotaka nafasi ya kwenda kujifunza katika kituo
hicho kwa kuwa wazazi wanawabana kupatamuda wa ziada ya kujifunza
Sayansi
“Mazingira tunayoishi inatufanya wasichana tusiwesawa na
wavulana katika kujifunza,ukiomba ruhusa kwenda kujifunza huwezi
kupewa,utaambiwa bora umsaidie Mama kazi hivyo kufanya mua wa kusoma
usiwepo lakini kwa wanaume iko tofauti akirudi hana kazi”alisema