Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwahutubia viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilayani Maswa katika mkutano uliofanyika uwanja wa Nguzo Nne mjini Maswa akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
(PICHA JOHN BUKUKU NA ADAM MZEE WA CCM)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Bi Shamsa Mohammed akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki Mh. Stanslaus Nyongo akielezea mafanikio ya maendeleo katika jimbo lake.
Picha mbalimbali zikionesha wana CCM mbalimbali waliohudhuria katika viwanja vya Nguzo Nne mjini Maswa kumsikiliza katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo aki msikiliza Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Bw.Ghalib Mkumbwa wakati alipotembelea kiwanda cha Chaki Maswa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo aki msikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Bw.Simon Berege wakati alipotembelea kiwanda cha Chaki Maswa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Bw.Simon Berege mara baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki Maswa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Kanali Ngemela Lubinga wakati walipotembelea kiwanda cha Chaki Maswa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila (kulia) alipokuwa akielezea sababu za kupanda kwa bei za bidhaa katika kijiji cha Njia Panda, kata ya Isanga, Maswa mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwasalimia wakazi wa kata ya Malampaka waliojitokeza barabarani na kusimamisha msafara wake.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa amekaa kwenye kigoda tayari kuvishwa vazi la heshima na Wazee wa shina namba 2, tawi la Shishiu wilayani Maswa mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza wakati wa kikao na wakazi wa shina namba 3, Songe kata ya Shanwa, Maswa ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama na shughuli za maendeleo mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi ya kituo cha afya Shishiu wilayani Maswa mkoa wa Simiyu.
………………………….
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo amewataka wazazi kupeleka watoto wa kike shule na siyo kuwalazimisha kuolewa ili mpate Ng’ombe kwakuwa watoto wakike siyo mtaji wa kujipatia Ngo’mbe.
Amesema kumekuwepo na tabia ya kuwabagua watoto wa kike na wa kiume na kutowapeleka shule watoto wa kike ili waolewe hili si jambo zuri katika jamii na linaharibu ustawi wa mtoto wa kike.
Chongolo ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilayani Maswa alipokuwa akiwahutubia katika mkutano uliofanyika uwanja wa Nguzo Nne mjini Maswa akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 wilayani humo.
“Serikali imejenga shule nyingi katika jimbo hili karibu kila kata ina sekondari ili watoto wa kike wasome kwani wasiposoma mnawageuza kuwa daraja la kuumizwa na kutumikishwa bila kuwa na uwezo wa kutafakari na kujiamulia mambo muhimu katika maisha yao, wapelekeni shule wasome kwani na wao wana uwezo wa kuwa na tija na msaada kama walivyo watoto wa kiume,” amesema Daniel Chongolo.
Amesisitiza kuwa uongozi ulipoewa dhamana ya kushughulika na suala la elimu katika mkoa wa Simiyu hakikisheni mnaratibu na kusimamia kikamilifu jambo hili ili watoto wa kike wapelekwe shule kwakuwa urithi wa msingi wa watoto ni elimu.
“Hata sisi wanaume tumeendelea siku hizi tunataka kuoa wanawake waliosoma wanaojitambua hatutaki wanawake wasiosoma wanaokaa tu nyumbani kusubiri waletewe pelekeni watoto wa kike shule,” amesema Daniel Chongolo